Kahama FM

Serikali wilayani Kahama imeipiga Marufuku kampuni ya QNET EAGLES UNITED inayojihusisha na biashara mtandaoni baada ya kubaini kufanya kazi bila kibali

19 May 2026, 3:02 pm

Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda akiwa katika eneo la tukio (Sebastian Mnakaya)

”kuanzia sasa hakuna kufanya biashara katika wilaya hii ya Kahama kwa kuwa hamna vibali pamoja na kuwatapeli wazazi na wanafunzi;

Serikali wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeipiga Marufuku kampuni ya QNET EAGLES UNITED inayojihusisha na biashara mtandaoni baada ya kubaini kufanya kazi bila kibali, pamoja na kuwarubuni Wanafunzi zaidi ya 50 kuacha vyuo mbambali kwa kuwahadaa kuwapatia ajira.

Ni katika Oparesheni hiyo, Maalum iliyotekelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Frank Nkinda inafanikiwa kuwamata baadhi ya viongozi wa Kampuni hii ambayo itajwa kufanya kazi bila kibali.

Aidha, Nkinda ameipiga marufuku kufanyakazi kwa kamuni hiyo katika wilaya ya Kahama, huku akielezea namba vijana hao wachuo walivyodanganywa na kuacha masomo yao.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Kahama

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi akiwemo Magreth Barnabas kutoka chuo cha TIA, Mariamu Juma chuo kuu Mzumbe na Emmanuel Masolwa kutoa chuo kikuu UDOM, ambapo wameeleza shubiri wanazopitia.

Sauti ya Magreth Barnabas, Mariamu Juma na Emmanuel Masolwa

Nae, Wankyo Warioba Mama Mzazi wa George Mwita aliyetapeliwa fedha, Kiongozi wa Kampuni ya QNET EAGLES LIMITED Laswai Laizer na Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyakato Hussen Mwita wameelezea hali ilivyokuwa kwa vijana hao.

Sauti za mzazi na mwenyekiti wa mtaa wa Nyakato Wankyo Warioba, Laswai Laizer na Hussen Mwita