Kahama FM
Kahama FM
12 May 2026, 4:03 pm

Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoa Shinyanga, wametaka kujua mpaka sasa maboma ambayo yameshajenga na yamefikia hatua gani ili wananchi wapate huduma za afya na shule.
Akizungumza katika cha baraza la madiwani katika kikao cha robo ya pili diwamani wa viti maalum Esther Matona, ambapa ametaka kujua mpaka sasa katika maboma yaliojengwa na wananchi katika sekta ya afya na elimu yamefikia wapi?

Akitoa ufafanuzi juu ya suala hilo, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ushetu Khadija Kaboleja, amesema kuwa mpaka sasa maboma 25 yameshakamilia, 14 yako katika hatua mbalimbali, huku maboma 6 yanatarajiwa kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2026/2026.

Awali, akisoma taarifa ya utekelezaji ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri hiyo, afisa mipango Shigela Ganja amesema kuwa serikali imeendelea kutekeleza ukamilishaji wa maboma, huku wananchi wakiendelea kujenga.