Kahama FM

Watanzania zaidi ya 100 waandaliwa kuendesha mradi EACOP

9 August 2026, 12:35 am

Viongozi mbalimbali kutoka wizara ya Nishati na EACOP wakikagua ujenzi wa kituo cha nne cha kusukuma mafuta(PS4) kilichoopo wilayani Mbongwe mkoani Geita (Picha na Sebastian Mnakaya)

ujenzi wa Kituo cha Nne cha Kusukuma Mafuta (PS4) ukifikia karibu asilimia 90 na mradi mzima upande wa Tanzania ukitarajiwa kukamilika ifikapo mwisho wa Desemba 2026

Zaidi ya Watanzania 100 tayari wamepatiwa mafunzo maalumu yatakayowawezesha kushiriki katika uendeshaji wa mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi Afrika Mashariki (EACOP) baada ya awamu ya ujenzi kukamilika, huku asilimia 82% ya wazawa wakifanya kazi katika mradi huo.

Hatua hiyo imekuja wakati utekelezaji wa mradi ukiwa umefikia hatua za mwisho, huku ujenzi wa Kituo cha Nne cha Kusukuma Mafuta (PS4) ukifikia karibu asilimia 90 na mradi mzima upande wa Tanzania ukitarajiwa kukamilika ifikapo mwisho wa Desemba 2026.

Hayo yamesemwa na Msimamizi wa mahudhui ya ndanikwa wazawa (Local Content katika EAOP), Neema Kweka, wakati wa ziara ya viongozi kutoka mradi waliotembela eneo hilo kukagua hatua za ujenzi wa kituo cha mafuta namba 4 kilichoopo katika kijiji cha Lubeho kata ya Nyakafuru wilayani Bongwe mkoani Geita.

Neema, amesema kuwa mkakati wa mradi haujaishia katika kutoa ajira kwa Watanzania, bali umejikita pia katika kuhakikisha ujuzi unaopatikana kupitia mradi huo unabaki nchini na kutumika katika miradi mingine.

Msimamizi wa mahudhui ya ndanikwa wazawa (Local Content katika EAOP) Neema Kweka

Aidha, amesema utekelezaji wa Local Content umejikita katika maeneo manne, ambayo ni ajira kwa Watanzania, kuwajengea ujuzi, kuhakikisha manunuzi yanafanyika ndani ya Tanzania na kujenga uwezo wa kampuni za wazawa.

Sauti ya Msimamizi wa mahudhui ya ndanikwa wazawa (Local Content katika EAOP) Neema Kweka

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na mradi huo akiwemo Paul Chesama na Eustace Majura, amesema kuwa wamenufaika na mradi huo kwa kupata ujuzi pamoja na ajira ambazo zimeweza kuwasaidia katika kujikwamua kiuchumi pamoja kufanya maendeleo

Sauti za wananchi Paul Chesama na Eustace Majura