Kahama FM

Cherehani aiomba halmashauri ya Ushetu kutenga eneo ujenzi wa kituo cha afya

July 12, 2023, 6:38 pm

Mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani akizungumza katika mkutano wa hadhara Kijiji Cha Ulowa picha na Sebastian Mnakaya

Kijiji cha Ulowa kina zahanati moja ambayo haikidhi mahitaji ya wananchi ambapo mbunge wa jimbo la Ushetu Emmannuel Cherehani ameiomba halmashauri kutafuta eneo la kujenga kituo cha afya chenye thamani ya shilingi milioni 500

Na Sebastian Mnakaya

Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeombwa kutafuta eneo la kujenga kituo cha afya chenye thamani ya shilingi milioni 500, katika kata ya Ulowa ili kupunguza wananchi kwenda umbali mrefu kupata matibabu.

Ombi hilo limetolewa na mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani wakati wa mkutano wa hadhara katika kata ya Ulowa, ambapo amesema kuwa kupitia kilimo cha tumbaku wakulima wanaingizia mapato mengi katika halmashauri hiyo na kati fedha hizo watenge ili kujenga kituo hicho cha afya.

Sauti ya mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani

Kwa upande wake diwani wa kata ya Ulowa Gabrela Kimaro amesema kuwa wananchi wa ulowa wanapata changamoto kubwa kutokana na kutokuwepo kwa kituo cha afya ambapo wanalazimika kwenda kata za jirani.

Sauti ya Diwani wa kata ya Ulowa Gabriela Kimaro

Nao, baadhi ya wananchi wa kata hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kuwa kukosekana kwa kituo cha afya katika kata hiyo imesababisha kinamama wajawazito kupata changamoto wakati wa kujifungua pamoja na kuomba serikali kujenga kituo hicho ili kupunguza changamoto wanazokutana nazo.

Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa halmashauri ya Ushetu akiwepo diwani wa kata ya Nyamilangano Robert Mihayo
Wananchi wa Kijiji Cha Ulowa wakiwa katika mkutano wa hadhara picha na Sebastian Mnakaya
Sauti za Wananchi wa Kijiji Cha Ulowa

Kata ya Ulowa ina zahanati moja, ambayo haikidhi huduma kutokana na kuwepo kwa watu wengi ambaao wanaishi katika kata hiyo hali inayosababisha kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya.