Kahama FM
Kahama FM
23 August 2026, 3:58 pm

‘‘Mwenge wa uhuru waweka jiwe la msingi katika ujenzi wa vumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Segese’’
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Wazo Mwang’onda ameipongeza Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kwa ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa katika shule ya Sekondari Segese iliyopo kijiji cha Busungo kwa gharama ya zaidi ya shilingi Milioni 45.5.
Mwang’onda ametoa pongezi hizo leo alipokuwa akiweka jiwe la msingi kwenye vyumba vya madarasa hayo ambavyo vinatarajia kukamilila mwezi Septemba mwaka huu, ambapo amesema Halmashauri hiyo imeanza kazi ya maandalizi kwaajili ya kupokea wanafunzi mwaka 2028 amvapo elimu imekuwa ya lazima kwa mtoto kusoma miaka kumi.
Aidha, Mwang’omba amempongeza mkurugenzi pamoja na tume yake kwa kuendelea kuteleza na kusimamia miradi vizuri, huku akiwataka kuendelea kutekeleza miradi mingine ka huu walioutekeleza.

Mkuu wa shule ya sekondari segese JohnMarry Prudence, aktoa taarifa kwa kiongozi huyo amesema shule hiyo ina wanafunzi 144 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne huku akieleza mradi umetekelezwa kwa force akaunt na wazabuni wa vifaa walipatikana kupitia mfumo wa manunuzi ya Umma (NeST).

Mbunge wa jimbo la Msalala Mabula Magangila amesema kuna shule za msingi 125 na sekondari 29 na mpango mkakati kila kijiji kuwe na shule ili watoto wasitembee umbali mrefu kutafuta elimu.