Kahama FM
Kahama FM
15 May 2026, 2:19 pm

”Wananchi kata ya Idahina wanahitaji nishati ya umeme kwenye maeneo ambayo tayari nguzo za umeme zimepita”
Wananchi wa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wameiomba serikali kupelekea nishati ya umeme katika laini kubwa ya umeme ili waendelee kukuza vipato vyao kwa kuazisha shughuli za kiuchumi zinazotegemea nishati hiyo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Diwani wa kata ya Idahina Mathias Makashi, wakati wa kikao cha robo ya pili katika baraza la madiwani ushetu, ambapo amesema kuwa lini wananchi watafikiwa na umeme kwenye maeneo ambayo umeme wa laini kubwa umepita.

Kwa upande wake, kaimu meneja wa TANESCO Halmashauri ya Ushetu Auxibius Magambo, amesema kuwa kwa sasa wanaanza kwenye maeneo ilipopita laini kumbwa kufunga Trasfoma ili wananchi waanze kupata umeme.
Katika awamu hii zaidi ya vijiji 52 katika halmashauri ya Ushetu vimeshapatiwa nishati ya umeme na serikali kiendelea kutekeleza kwa vijiji ambayo bado havijapatiwa umeme.