Kahama FM

Madiwani Ushetu watakiwa kuelimisha wananchi mvua za El Nino

2 September 2026, 2:38 pm

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Gagi Lala Gagi akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani (Picha na Sebastian Mnakaya)

Madiwani wa Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga wametakiwa kwenda kuwajengea uelewa wananchi wa Kata zao kuhusu uchukuaji wa tahadhari baada ya Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini -TMA kutangaza ujio wa mvua za juu ya wastani El Nino.

Tahadhari hiyo imetolewa hivi karibu na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) ya kuwataka wananchi kuchuka tahadhari juu ya mvua hizo, ikiwa pamoja na kutunza vyakula walivyovuna msimu huu.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Gagi Lala Gagi wakati wa kikao cha Maalum wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kwa ajili ya ufungaji wa Hesabu za Halmashauri, Afisa Kilimo wa Halmashauri hiyo Mapenzi Mshana akiwakumbusha wakulima kuendelea kujiandaa na msimu mpya wa kilimo kwa kufanya maandalizi ya mbegu za mazao zinazokubalika na hali hiyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Gagi Lala Gagi na Afisa Kilimo wa Halmashauri ya ushetu Mapenzi Mshana
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya ushetu Mapenzi Mshana

Kwa upande wao, baadhi ya diwani wa halmashauri hiyo akiwemo diwani wa Kata ya Kinamapula Samwel Sharif na diwani wa kata ya Igunda Tabu Katoto wameahidi kupeleka elimu hiyo kwa wananchi wao kwa njia ya kufanya mikutano ili kujiandaa na mvua za El Nino.

Sauti ya diwani wa Kata ya Kinamapula Samwel Sharif na diwani wa kata ya Igunda Tabu Katoto