Kahama FM
Kahama FM
19 October 2026, 12:27 pm

‘‘Serikali yaja na Mpango Kabambe wa Kidigitali kudhibiti ujenzi holela Kahama’’
Na Sebastian Mnakaya
Kwa miaka ya hivi karibuni, idadi ya wakazi katika Mji wa Kahama imeongezeka kwa kasi, hali iliyochangia kuongezeka kwa ujenzi holela.
Kutokana na hali hiyo, Serikali imeanzisha Mradi wa Mpango Kabambe wa Kidijitali utakaosaidia kudhibiti changamoto ya matumizi yasiyopangwa ya ardhi, kwa lengo la kuufanya Mji wa Kahama kuwa wa kisasa na wenye mpangilio mzuri.
Mpango huo pia unalenga kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi, ili kuwezesha maendeleo endelevu ya mji huo.