Chai FM

Recent posts

8 February 2022, 5:58 pm

Waandishi wawe chachu elimu dhidi ya vitendo vya ukatili

MBEYA Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Kaimu Afisa Elimu Mkoa Wilbrod Yanga amewataka Waandishi wa habari chipukizi ishirini na moja Mkoani Mbeya walionufaika na mradi wa SAUTI MPYA kuendeleza elimu waliyoipata baada ya mradi huo wa…

7 February 2022, 10:58 am

Wanafunzi waliomajumbani kwa changamoto za ujauzito warudi shule

MBEYA Serikali mkoani Mbeya kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amewataka wanafunzi waliomajumbani kwa changamoto za ujauzito kurudi kuendelea na masomo kwa utaratibu ambao serikali imeupanga. Homera ameyasema  kuwa serikali ya awamu ya sita kupitia kwa Rais…

2 February 2022, 6:01 am

Wizi wa pikipiki wakwamisha ndoto za vijana

RUNGWE-MBEYA Wananchi wa kata ya kawetele wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwa pamoja wameadhimia kuunda mpango wa pamoja wa kuanzisha ulinzi shirikishi (sungusungu) ndani ya kata hiyo kutokana na videndo vya wizi vinavyoendelea. kauli hiyo ya kuadhimia imekuja kwenye mkutano  ulioitishwa…

1 February 2022, 5:22 am

UWT Rungwe wapanda miti 50 kuendeleza uhifadhi wa Mazingira

RUNGWE-MBEYA Jumla ya miti hamsini imepandwa na Umoja wa wanawake  wa chama cha mapinduzi CCM(UWT) wilayani  Rungwe mkoani Mbeya katika Zahanati ya Suma pamoja na ofisi ya chama kwenye kata hiyo ikiwa ni maadhimisho ya miaka 45 tangu kuanziswa kwa…

29 January 2022, 7:26 am

Jamii ijitokeza kupata matibabu ugonjwa wa Ukoma

RUNGWE-MBEYA Jamii imetakiwa kujitokeza kupata matibabu pindi waonapo dalili za ugonjwa wa Ukoma hali itakayosaidia kuzuia maambukizi kwa wengine. Rai hiyo imetolewa na Mratibu wa kifua kikuu na Ukoma wilayani Rungwe Daktari Emmanuel Asukile alipokuwa akizungumzia kuelekea maadhimisho ya siku…

27 January 2022, 6:58 am

Abiria watoe taarifa kuepusha ajali barabarani

RUNGWE-MBEYA Tabia za kibinadamu zimepelekea kuongezeka kwa ajali barabarani kote nchini  hadi kufikia asilimia 76% kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa hivi karibuni na jeshi la polisi. Akizungumza na Radio cha FM kupitia kipindi cha Amka na Chai Mkuu wa kikosi…

26 January 2022, 8:50 am

Wananchi waitumie wiki ya sheria kupata msaada wa kisheria

RUNGWE-MBEYA Kuelekea kilele cha wiki ya sheria nchini mahakama wilayani Rungwe imewataka wananchi kujitokeza katika maeneo ambayo zoezi la utoaji elimu litakuwa likifanyika . Akizungumza na Radio Chai Kaimu Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Rungwe Bw.Augustine Lugome amesema  utaratibu huu …

3 January 2022, 9:46 am

Madarasa 24 yakamilikika kwa asilimia 100

RUNGWE-MBEYA Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Busokelo Bi, LOEMA PETER  amekabidhi takribani vyumba vya madarasa 24 kwa Mkuu wa wilaya ya Rungwe  baada ya kumalika ndani ya muda ulio pangwa. Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na kituo hiki huku akieleza…

24 December 2021, 5:45 am

Umbali chazo cha unyanyasaji wilayani Rungwe

Umbali wa malezi uliopo baina ya wazazi, walezi, walimu na watoto imetajwa kuwa moja kati ya sababu zinazopelekea kushamiri kwa vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto wilayani Rungwe mkoani Mbeya. Aidha jamii imetakiwa kuwalinda zaidi watoto huku wazazi wakitakiwa kujenga…

Kuhusu Chai FM

Chai FM radio ni radio inayomilikiwa na Umoja wa wakulima wa Chai Rungwe, Ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha mkulima wa Chai wilaya ya Rungwe anapata taarifa sahihi ambazo zitasaidia kuendeleza zao la Chai pamoja na shughuli zake za kiuchumi, Elimu na Kijamii.

Uwepo wa radio Chai FM umesaidia mkulima wa zao la Chai wilaya ya Rungwe kupata taarifa kwa wakati zinazohusu zao la chai na mwenendo wake pamoja na elimu juu ya kilimo biashara kwa zao la chai na mazao mengine pamoja na ufugaji.

Hii ni kutokana na uguu wa kufikisha taarifa ya masuala ya kilimo kwa wakulima wa chai jiografia ya wilaya ikiwa ni kikwazo kwa wakulima kupata taarifa mbalimbali za ndani na nje ya wilaya pamoja na mpango wa kilimo endelevu.

Dira

Kuona jamii ya wakulima na wafugaji wa wilaya ya Rungwe wanakuwa na maisha bora

Dhamira

Kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Wilaya ya Rungwe kuelimisha na kutoa taarifa za kilimo, mifugo, biashara,viwanda na habari za kijamii kupitia vipindi vya redio.

Chai Fm Radio inasikika maeneo tofauti kama ifuatavyo

Mkoa wa Mbeya – Wilaya za Rungwe, Busokelo, Kyela, na Mbeya Vijijini kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Njombe – Wilaya za Makete, Ludewa

Mkoa wa Songwe – Wilaya za Ileje na Songwe kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Ruvuma – Wilaya za Mbinga na Nyasa.

Lakini pia chai Fm inapatikana ukiwa popote duniani kupitia radiotadio.co.tz/chaifm/