Chai FM

Recent posts

16 December 2021, 2:27 pm

Vitabu zaidi ya elfu tatu vyapokelewa Rungwe

RUNGWE. Katika kuboresha mazingira ya elimu nchini wadau mbalimbali wa elimu wameshauriwa kusaidia vifaa mbalimbali kama vile vitabu vya kiada na ziada. Akizungumza mara baada ya kupokea vitabu kutokea taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Sakyambo interprisess yenye makao makuu yake…

14 December 2021, 5:14 am

Jamii iwatembelee watu wenye uhitaji

RUNGWE-MBEYA Wazazi na walezi wameaswa kuwajali  na kuwathamini watu wenye uhitaji kwa kutoa mahitaji muhimu kwa watoto hao ikiwemo kuwatembelea katika maeneo mbalimbali kwani itasaidia kuongeza faraja kwao. Hayo yamezungumzwa  na Umoja wa akina mama kutoka Katumba walipo watembelea watoto…

28 November 2021, 8:42 am

Serikali kutenga fedha kwajili ya kuboresha miundombinu ya maji Rungwe

RUNGWE-MBEYA Mbunge wa jimbo la Rungwe  ANTON  MWANTONA amesema tatizo la maji linalo wakabili wanachi wa jimbo la Rungwe linaenda kumalizika baada ya serikali kutenga fedha kwajili ya kuboresha miundombinu ya maji kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungunza na na…

28 November 2021, 8:37 am

Wizara ya Elimu itenge fedha kwajili ya  ukarabati wa shule kongwe nchini

RUNGWE-MBEYA Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania KASSIM  MAJALIWA ameagiza wizara ya Elimu kutenga fedha kwajili ya  ukarabati wa shule zote kongwe nchini. Maagizo hayo ameyatoa wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali Mkoani Mbeya wilayani Rungwe Novemba…

23 November 2021, 9:34 am

TANLAP yawajengea uwezo wasaidizi wa kisheria Rungwe

RUNGWE Kaimu mkurugenzi kutoka mtandao wa Mashirika yanayotoa msaada wa kisheria Tanzania [TANLAP] MCHELELI MACHUMBANA ameitaka jamii kujua sheria mbambali ili kukabiliana na unyanyasaji uliopo kwenye maeneo yao. Ametoa kauli hiyo mbele ya wasaidizi wa kisheria waliopo wilayani Rungwe mkoani…

22 November 2021, 9:36 am

Mafunzo yawe chachu ya mabadiliko

RUNGWE-MBEYA NA:STAMILY MWAKYOMA Vijana wametakiwa kuwa vielelezo katika jamii kupitia mafunzo yanayotolewa na vyuo vya maendeleo ya wananchi hapa nchini. Kauli hiyo imetolewa na mgeni rasmi Ndugu Gerald Kimbunga  katika maafali ya 45 ya chuo cha maendeleo ya Wananchi Katumba…

15 November 2021, 3:09 pm

Jamii imetakiwa kusaidia watoto wenye uoni hafifu

RUNGWE-MBEYA Mwenyekiti wa chama wasioona (TLB )mkoa wa Mbeya ndg.YOHANA MONGA amewaomba wadau mbalimbali kote nchini kusaidia vifaa vya kufundishia watoto wenye mahitaji maalum mashuleni. Ametoa kauli hiyo alipokuwa akikabidhi fimbo nyeupe kwa wanafunzi wasioona kwenye shule ya mahitaji maalum…

12 November 2021, 4:59 am

34 Wahitimu mafunzo ya Jeshi la akiba wilayani Rungwe

RUNGWE-MBEYA Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mh,Rashidi Chuachua amewaomba wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba [mgambo]wilayani Rungwe kuenda kuyaishi yale yote waliofundishwa wakiwa mafunzoni. Ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya Jeshi hilo la akiba mwaka 2021 katika halmashauri ya…

10 November 2021, 5:57 am

4326 kufanya mtihani wa kidato Cha nne Rungwe

Jumla ya wanafunzi 4,326 wilayani Rungwe mkoani Mbeya wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne unaotarajiwa kuanza tarehe 15.11.2021 kote nchini. Kwa mujibu wa Afisa elimu sekondari wilayani Rungwe Mwl. Yona Mwaisaka amesema kati ya watahiniwa hao 231 ni…

9 November 2021, 6:09 pm

Makusanyo hafifu ya mapato yawafukuzisha kazi watendaji

KYELA-MBEYA Halmashauri ya wilaya ya kyela mkoani Mbeya imeagizwa kuwafuta kazi watendaji wa kata  ambao kata zao zimekuwa za mwisho kwenye zoezi la ukusanyaji wa mapato. Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera mbele ya baraza…

Kuhusu Chai FM

Chai FM radio ni radio inayomilikiwa na Umoja wa wakulima wa Chai Rungwe, Ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha mkulima wa Chai wilaya ya Rungwe anapata taarifa sahihi ambazo zitasaidia kuendeleza zao la Chai pamoja na shughuli zake za kiuchumi, Elimu na Kijamii.

Uwepo wa radio Chai FM umesaidia mkulima wa zao la Chai wilaya ya Rungwe kupata taarifa kwa wakati zinazohusu zao la chai na mwenendo wake pamoja na elimu juu ya kilimo biashara kwa zao la chai na mazao mengine pamoja na ufugaji.

Hii ni kutokana na uguu wa kufikisha taarifa ya masuala ya kilimo kwa wakulima wa chai jiografia ya wilaya ikiwa ni kikwazo kwa wakulima kupata taarifa mbalimbali za ndani na nje ya wilaya pamoja na mpango wa kilimo endelevu.

Dira

Kuona jamii ya wakulima na wafugaji wa wilaya ya Rungwe wanakuwa na maisha bora

Dhamira

Kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Wilaya ya Rungwe kuelimisha na kutoa taarifa za kilimo, mifugo, biashara,viwanda na habari za kijamii kupitia vipindi vya redio.

Chai Fm Radio inasikika maeneo tofauti kama ifuatavyo

Mkoa wa Mbeya – Wilaya za Rungwe, Busokelo, Kyela, na Mbeya Vijijini kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Njombe – Wilaya za Makete, Ludewa

Mkoa wa Songwe – Wilaya za Ileje na Songwe kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Ruvuma – Wilaya za Mbinga na Nyasa.

Lakini pia chai Fm inapatikana ukiwa popote duniani kupitia radiotadio.co.tz/chaifm/