Chai FM

Recent posts

27 October 2021, 5:22 am

Milioni 500 kusaidia upatakanaji wa Maji Rungwe

RUNGWE. Ofisi ya mamlaka ya maji Tukuyu Wilayani Rungwe mkoani Mbeya imeahidi kutatua changamoto ya maji kwa wananchi kupitia miradi inayoenda kutekelezwa ndani ya Wilaya. Kupitia Meneja wa mamlaka ya maji Tukuyu  Peter Amon amesema hayo akizungumza na Radio Chai…

26 October 2021, 9:07 am

Jamii iwe makini wizi mtandaoni

RUNGWE Jeshi la polisi Wilayani Rungwe limewaomba wafanyabishara kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kukabiliana na watu wanao jihusisha na uwizi wa mtandaoni. Jeshi hilo limetoa kauli hiyo kupitia Mkuu wa upelezi Wilaya ya Rungwe WILLIAM NYAMAKOMANGO alipokutana na wafanyabiashara kwenye…

25 October 2021, 9:43 am

Matumizi sahihi ya mswaki tiba ya kinywa

RUNGWE Mratibu wa afya ya kinywa na meno Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya DOKT HOSEA MWAKYUSA ameelezea matumizi sahihi ya miswaki ambapo mswaki unatakiwa kutumika ndani ya miezi mitatu. Akizungumza na kituo hiki amesema kuwa kinywa ni kitu muhumu katika kiungo…

25 October 2021, 9:21 am

Machinga kutii agizo la serikali

RUNGWE Wafanya biashara wadogo (machiga) soko la Tukuyu, wamesema wameanza kutekeleza agizo la Halmashauri la kuhama katika maeneo yasiyo rasmi wanayo fanyia biashara zao na badala yake wahamie katika maeneo waliyo pangiwa na halmashauri. Wameyasema hayo wakati wakizungumza na radio…

21 October 2021, 12:09 pm

Mseleleko wawaponza vijana VVU

RUNGWE Vijana wilayani Rungwe Mkoani Mbeya wameelezea sababu zinazo pelekea baadhi ya vijana kupata maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi kutokana na tafiti zilizotolewa na tume ya kudhibiti Ukimwi nchini (Tacaids). Tafiti hizo za mwaka 2020 zimebainisha kuwa vijana kati…

21 October 2021, 9:33 am

Mila na desturi zinavyokandamiza wagonjwa wa akili

RUNGWE Hivi karibuni Dunia imeadhimisha siku ya magonjwa ya afya ya akili jamii wilayani Rungwe Mkoani Mbeya ametakiwa kuachana na imani za kishirikiana juu ya ugonjwa huo. Akizungumza na kituo hiki mratibu wa afya ya akili wilaya Dkt JOHN DUNCAN…

13 October 2021, 8:56 am

Wivu wawanyima uhuru watumishi

RUNGWE-MBEYA Wivu wa maendeleo imetajwa kuwa moja kati ya sababu zinazopelekea waajiri wengi wa wafanyakazi wa majumbani kutowaruhusu wafanyakazi wao kuendesha miradi yao. Wakizungumza na waandishi wetu baadhi ya wananchi wilayani hapa wamesema kwamba baadhi ya waajiri wanaogopa kuzidiwa kipato…

Kuhusu Chai FM

Chai FM radio ni radio inayomilikiwa na Umoja wa wakulima wa Chai Rungwe, Ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha mkulima wa Chai wilaya ya Rungwe anapata taarifa sahihi ambazo zitasaidia kuendeleza zao la Chai pamoja na shughuli zake za kiuchumi, Elimu na Kijamii.

Uwepo wa radio Chai FM umesaidia mkulima wa zao la Chai wilaya ya Rungwe kupata taarifa kwa wakati zinazohusu zao la chai na mwenendo wake pamoja na elimu juu ya kilimo biashara kwa zao la chai na mazao mengine pamoja na ufugaji.

Hii ni kutokana na uguu wa kufikisha taarifa ya masuala ya kilimo kwa wakulima wa chai jiografia ya wilaya ikiwa ni kikwazo kwa wakulima kupata taarifa mbalimbali za ndani na nje ya wilaya pamoja na mpango wa kilimo endelevu.

Dira

Kuona jamii ya wakulima na wafugaji wa wilaya ya Rungwe wanakuwa na maisha bora

Dhamira

Kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Wilaya ya Rungwe kuelimisha na kutoa taarifa za kilimo, mifugo, biashara,viwanda na habari za kijamii kupitia vipindi vya redio.

Chai Fm Radio inasikika maeneo tofauti kama ifuatavyo

Mkoa wa Mbeya – Wilaya za Rungwe, Busokelo, Kyela, na Mbeya Vijijini kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Njombe – Wilaya za Makete, Ludewa

Mkoa wa Songwe – Wilaya za Ileje na Songwe kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Ruvuma – Wilaya za Mbinga na Nyasa.

Lakini pia chai Fm inapatikana ukiwa popote duniani kupitia radiotadio.co.tz/chaifm/