Chai FM

Recent posts

9 May 2024, 2:12 pm

Kipindi kuhusu mashauri ya ndoa

Katika kipindi hiki ni mwendelezo wa elimu ya msaada wa kisheria mada kuu ni muongozo wa watumiaji wa mahakama, hapa utasikiliza zaidi mashauri ya ndoa ikiwa ni pamoja na usuluhishi wa ndoa.

9 May 2024, 1:16 pm

Jamii kukabiliana na ukatili mtandaoni Rungwe

Kutokana na kuwepo kwa vitendo vya ukatili mtandaoni dhidi ya watoto wazazi na walezi watakiwa kuwa mstari wa mbele katika malezi kwa watoto Na Noah Kibona Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu imeendesha kampeni maalumu dhidi…

1 May 2024, 6:47 pm

Serikali kuagiza kuundwa kwa mabaraza sherehe za mei mosi

ili kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji wa kinjisia mahala pakazi mabaraza yametakiwa kuamzisha lengo ni kukabiliana na changamoto kwa watumishi. Rungwe-Mbeya Na Lennox Mwamakula Serikali imeziagiza taasisi zote umma na binafsi kuunda mabaraza kwenye taasisi hizo ili kuwawezesha watumishi  wao…

30 April 2024, 6:59 pm

Wananchi wafurahia ujenzi wa barabara ya katumba-mwakaleli

serikali imeendelea kuboresha miundombiu ya barabara kwa dhumuni ya kuunganisha halmashauri zote nchini ili kuweza kufikika kwa urahisi wananchi wakiwa kwenye furaha baada ya mkandarasi kukabidhiwa barabara ili anze kujenga [picha na lennox mwamakula] RUNGWE-MBEYA Na lennox Mwamakula Serikali imetenga…

26 April 2024, 2:59 pm

Wanafunzi kumaliza vitendo vya ukatili shuleni

Vijana wametakiwa kuwa msitari wa mbele kutoa taarifa oindi wanapo fanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia MBEYA Na Lennox Mwamakula Kutokana na ongezeko la vitendo vya ukatili vinavyoripotiwa kwenye maeneo mbalimbali mkoani mbeya, serikali kwa kushrikiana na wadau mbalimbali wamekutana…

26 April 2024, 2:09 pm

Jamii yatakiwa kutunza mazingira Rungwe

katibu tawala wa wilaya ya Rungwe Ally Kiumwa akisoma taarifa mbele ya mkuu wa wilaya kwenye siku ya maadhimisho ya miaka 60 ya muungano [picha na Lennox Mwamakula] wananchi wametakiwa kuendelea kudumisha amani iliyopo kwa kulinda muungano wa tanzania RUNGWE-MBEYA…

25 April 2024, 1:49 am

Dsw kuimarisha mifumo ya kuzuia ukatili wa kijinsia

ili kukabiliana na vitendo ya ukatili wa kijinsia kwa watoto jamii imetakiwa kuwa mstari wa mbele kutoa tarifa kwenye vyombo vya kisheria. MBEYA Na Lennox Mwamakula Shirika lisilo la kiserikali la DSW Tanzania linalojihusisha na masuala ya maendeleo Kwa vijana…

23 April 2024, 4:08 pm

Wasichana 21,094 kupatiwa chanjo ya HPV Rungwe

Halmshauri ya wilaya ya Rungwe imekusudia kuwalinda watoto wa kike wenye umri wa kuanzia miaka 9-14 kwa kuwapatia chanjo ya kupambana na saratani ya mlango wa kizazi (HPV) Na Judith Mwakibibi Mkuu wa wilaya ya Rungwe Jaffar Haniu amewataka maafisa…

19 April 2024, 3:16 pm

Vitendo vya wizi vyaongezeka Rungwe

Jamii imeshauriwa kutoa taarifa kwenye viongozi wa maeneo yao bindi wanapo ona vyaashiria ya uwizi au uvunjifu wa amani kwenye maeneo yao. NA lennox Mwamakula Wananchi wa mtaa wa Mpindo uliopo kata ya Bulyaga wilayani  Rungwe wamekubaliana kuanzisha ulinzi shirikishi…

4 April 2024, 6:45 pm

Baada ya daraja kubomoka wananchi wakosa huduma Rungwe

wananchi wakishuhudia daraja likisobwa na maji baada ya mvua kunyesha[picha na Lennox Mwamakula] Jamii imeshauriwa kutolima kwenye vyanzo vya maji kwani kunapelekea madhara makubwa kwenye shughuli za kibinadamu. Rungwe-Mbeya Na lennox Mwamakula Wananchi wilayani Rungwe wameiomba serikali kuwajengea daraja lililo…

Kuhusu Chai FM

Chai FM radio ni radio inayomilikiwa na Umoja wa wakulima wa Chai Rungwe, Ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha mkulima wa Chai wilaya ya Rungwe anapata taarifa sahihi ambazo zitasaidia kuendeleza zao la Chai pamoja na shughuli zake za kiuchumi, Elimu na Kijamii.

Uwepo wa radio Chai FM umesaidia mkulima wa zao la Chai wilaya ya Rungwe kupata taarifa kwa wakati zinazohusu zao la chai na mwenendo wake pamoja na elimu juu ya kilimo biashara kwa zao la chai na mazao mengine pamoja na ufugaji.

Hii ni kutokana na uguu wa kufikisha taarifa ya masuala ya kilimo kwa wakulima wa chai jiografia ya wilaya ikiwa ni kikwazo kwa wakulima kupata taarifa mbalimbali za ndani na nje ya wilaya pamoja na mpango wa kilimo endelevu.

Dira

Kuona jamii ya wakulima na wafugaji wa wilaya ya Rungwe wanakuwa na maisha bora

Dhamira

Kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Wilaya ya Rungwe kuelimisha na kutoa taarifa za kilimo, mifugo, biashara,viwanda na habari za kijamii kupitia vipindi vya redio.

Chai Fm Radio inasikika maeneo tofauti kama ifuatavyo

Mkoa wa Mbeya – Wilaya za Rungwe, Busokelo, Kyela, na Mbeya Vijijini kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Njombe – Wilaya za Makete, Ludewa

Mkoa wa Songwe – Wilaya za Ileje na Songwe kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Ruvuma – Wilaya za Mbinga na Nyasa.

Lakini pia chai Fm inapatikana ukiwa popote duniani kupitia radiotadio.co.tz/chaifm/