Chai FM

Recent posts

16 December 2022, 12:09 pm

Usafi kiboko ya magonjwa ya mlipuko

RUNGWE- MBEYA NA: SABINA MARTIN Msimu huu wa mvua zilizoanza kunyesha wilayani Rungwe mkoani Mbeya wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari na kuzingatia afua za afya ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu. Akizungumza na Chai FM ofisini kwake afisa…

16 December 2022, 11:53 am

Matumizi ya dawa kiholela chanzo cha magonjwa sugu

  RUNGWE, Imeelezwa kuwa matumizi ya dawa za binadamu bila kufuata ushauri wa daktari ni chanzo cha usugu wa magonjwa na hatimaye kupelekea kifo. Hayo yamesemwa na mganga mkuu wa Wilaya ya Rungwe Dkt Diokles Ndaiza wakati akizungumza na Chai…

12 October 2022, 4:08 pm

Siku ya kimataifa ya mtoto wa kike wazazi wameaswa kuwa karibu na watoto

RUNGWE-MBEYA NA: SABINA MARTIN Wazazi na walezi wilayani Rungwe mkoani Mbeya wametakiwa kutenga muda wa kukaa na kuzungumza na watoto wao kuhusu mambo mbali mbali ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili vinavyoendelea katika jamii. Rai hiyo imetolewa na baaadhi ya…

12 October 2022, 3:56 pm

wakulima wilayani Rungwe wametakiwa kutumia mbolea kwa usahihi

RUNGWE-MBEYA NA:SABINA MARTIN Kuelekea madhimisho ya siku ya mbolea duniani ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo octoba 13 wakulima wilayani hapa wametakiwa kutumia mbolea kwa usahihi ili kupata mazao mengi. Akizungumza kwa njia ya simu na Chai FM  afisa kilimo wilayani…

23 September 2022, 5:41 am

Jamii imetakiwa kusalimisha silaha haramu

RUNGWE-MBEYA NA,JUDITH MWAKIBIBI Kutokana na kampeni inayoendelea ya usalimishaji wa silaha kitaifa wananchi wilayani Rungwe mkoani Mbeya wametakiwa kusalimisha silaha haramu zinazomilikiwa kinyume na utaratibu. Akizungumza  katika studio za radio chai FM mrakibu wa jeshi   la polisi Wilayanl ya Rungwe…

12 September 2022, 5:26 pm

Bei ya ndizi kushuka kilio kwa wakulima

RUNGWE-MBEYA, NA:LOVENESS RAJABU Wafanyabiashara wa ndizi wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wameeleza bei ya ndizi kwa kipindi hiki cha kiangazi. Wakizungumza na Chai FM wafanyabiashara wa ndizi katika soko la Mabonde wamesema kuwa kwa sasa bei ya ndizi ipo chini…

10 September 2022, 9:26 am

TOZO ya miamala ya simu yasaidia upatikanaji wa madarasa

RUNGWE-MBEYA Kupitia TOZO ya miamala ya simu, Serikali imetoa jumla ya shilingi Million 12.5 kwa ajili ya ukamilishaji wa chumba Cha darasa katika shule ya Sekondari Ndembela one iliyopo kata ya Makandana. Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe imetoa kiasi…

10 September 2022, 7:47 am

Jamii iwapeleke watoto wapate chanjo ya polio

RUNGWE-MBEYA NA:WANDE BUSHU Mratibu Wa Chanjo Katika Halmashauri Ya  Wilaya Rungwe Mkoani   Mbeya Ezekiel Mvile Amewaomba Wazazi Kuwapeleka Watoto Wao Katika Vituo Vya Afya  Waweze Kukamilisha  Dozi Ya Polio ili Iweze Kuwakinga Na Ugonjwa Huo. Ameyasema Hayo Wakati Akizungumza Na…

10 September 2022, 7:43 am

Wananchi Rungwe mjitokeze kuupokea Mwenge

RUNGWE-MBEYA. NA:JUDITH MWAKIBIBI Wananchi wilayani RUNGWE MKOANI MBEYA wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kuupokea mwenge wa uhuru utakaofika 10sept 2022 ilikuweza kuzindua miradi mbalimbali katika halmashauri. Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Rungwe Dk Vicent Anney alipokuwa ametembelea…

9 September 2022, 10:15 am

kilio uhaba wa maji Rungwe kupata tiba mwezi oktoba

RUNGWE-MBEYA NA:WANDE BUSHU Wananchi wa Kitongoji cha Kawetele chini Wilaya ya  Rungwe Mkoani Mbeya wameiomba serikali kuwatatulia changamoto ya huduma ya maji iliyo dumu kwa muda mrefu licha la kulipia bili ya maji kila mwezi Wakizungumza na Chai Fm wamesema …

Kuhusu Chai FM

Chai FM radio ni radio inayomilikiwa na Umoja wa wakulima wa Chai Rungwe, Ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha mkulima wa Chai wilaya ya Rungwe anapata taarifa sahihi ambazo zitasaidia kuendeleza zao la Chai pamoja na shughuli zake za kiuchumi, Elimu na Kijamii.

Uwepo wa radio Chai FM umesaidia mkulima wa zao la Chai wilaya ya Rungwe kupata taarifa kwa wakati zinazohusu zao la chai na mwenendo wake pamoja na elimu juu ya kilimo biashara kwa zao la chai na mazao mengine pamoja na ufugaji.

Hii ni kutokana na uguu wa kufikisha taarifa ya masuala ya kilimo kwa wakulima wa chai jiografia ya wilaya ikiwa ni kikwazo kwa wakulima kupata taarifa mbalimbali za ndani na nje ya wilaya pamoja na mpango wa kilimo endelevu.

Dira

Kuona jamii ya wakulima na wafugaji wa wilaya ya Rungwe wanakuwa na maisha bora

Dhamira

Kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Wilaya ya Rungwe kuelimisha na kutoa taarifa za kilimo, mifugo, biashara,viwanda na habari za kijamii kupitia vipindi vya redio.

Chai Fm Radio inasikika maeneo tofauti kama ifuatavyo

Mkoa wa Mbeya – Wilaya za Rungwe, Busokelo, Kyela, na Mbeya Vijijini kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Njombe – Wilaya za Makete, Ludewa

Mkoa wa Songwe – Wilaya za Ileje na Songwe kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Ruvuma – Wilaya za Mbinga na Nyasa.

Lakini pia chai Fm inapatikana ukiwa popote duniani kupitia radiotadio.co.tz/chaifm/