Chai FM

Recent posts

10 September 2022, 9:26 am

TOZO ya miamala ya simu yasaidia upatikanaji wa madarasa

RUNGWE-MBEYA Kupitia TOZO ya miamala ya simu, Serikali imetoa jumla ya shilingi Million 12.5 kwa ajili ya ukamilishaji wa chumba Cha darasa katika shule ya Sekondari Ndembela one iliyopo kata ya Makandana. Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe imetoa kiasi…

10 September 2022, 7:47 am

Jamii iwapeleke watoto wapate chanjo ya polio

RUNGWE-MBEYA NA:WANDE BUSHU Mratibu Wa Chanjo Katika Halmashauri Ya  Wilaya Rungwe Mkoani   Mbeya Ezekiel Mvile Amewaomba Wazazi Kuwapeleka Watoto Wao Katika Vituo Vya Afya  Waweze Kukamilisha  Dozi Ya Polio ili Iweze Kuwakinga Na Ugonjwa Huo. Ameyasema Hayo Wakati Akizungumza Na…

10 September 2022, 7:43 am

Wananchi Rungwe mjitokeze kuupokea Mwenge

RUNGWE-MBEYA. NA:JUDITH MWAKIBIBI Wananchi wilayani RUNGWE MKOANI MBEYA wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kuupokea mwenge wa uhuru utakaofika 10sept 2022 ilikuweza kuzindua miradi mbalimbali katika halmashauri. Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Rungwe Dk Vicent Anney alipokuwa ametembelea…

9 September 2022, 10:15 am

kilio uhaba wa maji Rungwe kupata tiba mwezi oktoba

RUNGWE-MBEYA NA:WANDE BUSHU Wananchi wa Kitongoji cha Kawetele chini Wilaya ya  Rungwe Mkoani Mbeya wameiomba serikali kuwatatulia changamoto ya huduma ya maji iliyo dumu kwa muda mrefu licha la kulipia bili ya maji kila mwezi Wakizungumza na Chai Fm wamesema …

9 September 2022, 9:57 am

Jamii itoe taarifa kuhusu vitendo vya ukatili

RUNGWE-MBEYA. NA:LETHISIA SHIMBI Baadhi ya Wanawake Wilayani Rungwe mkoani Mbeya  wameeleza namna wanavyoshiriki kutoa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo. Wakizungumza na chai fm BAHATI SIMON na MAIDASI NDAMU wamesema endapo vitendo…

9 September 2022, 9:51 am

wakulima elfu 17 tayari wamesajiliwa Mbolea ya ruzuku

RUNGWE-MBEYA NA:LETHISIA SHIMBI Wakulima wilayani rungwe Mkoani mbeya wametakiwa  kufuata taratibu  wa kujisajili  kwenye mfumo Ili kuweza kupata Ruzuku za pembejeo. Akizungumza na kituo Chai FM  afisa kilimo wilayani  hapa JUMA MZARA amesema katika halmashauri ya Rungwe wamesajiri wakulima elfu…

26 May 2022, 9:49 am

RUNGWE-MBEYA NA:LETHISIA SHIMBI Jamii wilayani Rungwe mkoani Mbeya imetakiwa kuachana na mtazamo hasi kuhusu watu wenye ulemavu badala yake wametakiwa kujumuika kwa pamoja na kushirikiana katika mambo mbalimbali. Rai hiyo imetolewa na Meneja wa shirika la TRAIDCRAFT EXCHARGE Ndg Ledis…

25 May 2022, 10:24 am

Wafanyabiashara 1800 Rungwe wanufaika na mafunzo.

  RUNGWE-MBEYA NA:BETRIDA ANYEGILE Wafanyabiashara elfu moja na mia nane kutoka kata takribani kumi Wilayani Rungwe  Mkoani Mbeya wamepatiwa mafunzo ya urasimishaji biashara na  Mpango wa kurasimisha rasirimali na biashara Tanzania ( MKURABITA). Akizungumza na vyombo vya habari katika kufunga…

19 May 2022, 2:22 pm

Mkurabita awa Mkombozi kwa wafanyabiashara

Wafanyabiashara Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya wametakiwa kurasimisha shughuli zao za biashara ili kupanua wigo wa kuzifikia fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na urahisi wa kupata mikopo na leseni za biashara. Hayo yamejiri katika ufunguzi wa mafunzo ya kurasimisha biashara za…

Kuhusu Chai FM

Chai FM radio ni radio inayomilikiwa na Umoja wa wakulima wa Chai Rungwe, Ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha mkulima wa Chai wilaya ya Rungwe anapata taarifa sahihi ambazo zitasaidia kuendeleza zao la Chai pamoja na shughuli zake za kiuchumi, Elimu na Kijamii.

Uwepo wa radio Chai FM umesaidia mkulima wa zao la Chai wilaya ya Rungwe kupata taarifa kwa wakati zinazohusu zao la chai na mwenendo wake pamoja na elimu juu ya kilimo biashara kwa zao la chai na mazao mengine pamoja na ufugaji.

Hii ni kutokana na uguu wa kufikisha taarifa ya masuala ya kilimo kwa wakulima wa chai jiografia ya wilaya ikiwa ni kikwazo kwa wakulima kupata taarifa mbalimbali za ndani na nje ya wilaya pamoja na mpango wa kilimo endelevu.

Dira

Kuona jamii ya wakulima na wafugaji wa wilaya ya Rungwe wanakuwa na maisha bora

Dhamira

Kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Wilaya ya Rungwe kuelimisha na kutoa taarifa za kilimo, mifugo, biashara,viwanda na habari za kijamii kupitia vipindi vya redio.

Chai Fm Radio inasikika maeneo tofauti kama ifuatavyo

Mkoa wa Mbeya – Wilaya za Rungwe, Busokelo, Kyela, na Mbeya Vijijini kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Njombe – Wilaya za Makete, Ludewa

Mkoa wa Songwe – Wilaya za Ileje na Songwe kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Ruvuma – Wilaya za Mbinga na Nyasa.

Lakini pia chai Fm inapatikana ukiwa popote duniani kupitia radiotadio.co.tz/chaifm/