Chai FM

Shilingi milioni 90 kuboresha miundombinu Lupata

7 June 2024, 10:25 am

Ili kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kupata elimu katika mazingira mazuri serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya elimu nchini.

RUNGWE-MBEYA

Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo  katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo.

Mhe. Homera leo 05/06/2024 amefanya ziara ya kukagua miradi wa ukarabati miundombinu katika shule ya msingi Lupata iliyoko katika kijiji cha Lupata Kata ya Lupata.

Shule ya Msingi Lupata ilipokea shilingi Milioni 90,kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu shuleni hapo ambayo ni  ,vyumba vinne vya madarasa na ofisi mbili.

Hadi sasa ujenzi umefikia aslimia 98 na  fedha iliyotumika ni shilingi Millioni 73,6.

Mhe.Homera aipongeza Halmashauri ya Busokelo namna inavyosimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuzingatia matumizi sahihi ya fedha na kushurikiana na Serikali ya Kijiji cha Lupata pamoja na kamati ya Ujenzi ili kufanikia utekelezaji miradi ya maendeleo.

Aidha Shilingi Milioni 16.3 zimebaki na zimeelekezwa kutumika Kujenga  matundu matano (5) ya vyoo vya Wasicha na tundu moja la choo cha Wanafunzi Wavulana wenye mahitaji Maalumu.