Chai FM

Wafanyabiashara wakerwa na takataka ndani ya soko Rungwe

25 March 2025, 11:33 am

Serikali imetakiwa kuwa mstari wa mbele kuboresha miundombinu ya masoko

RUNGWE -MBEYA

Na Neema Nyirenda

Serikali imeombwa kuboresha miundombinu ya  masoko yote nchini kwani kutasaidia kuinua uchumi wa watumiaji wa masoko hayo na Taifa kwa ujumla

Hayo yameelezwa na wafanyabiashara wa ndizi soko la mabonde lililopo kata ya Msasani wilayani Rungwe mkoani Mbeya

Wafanyabiashara  hao  wameeleza changamoto wanazokumbana nazo katika soko hilo ikiwemo wingi wa taka ambazo ni kero kwa utendaji wa biashara zao na hatarishi kwa afya zao.

viongozi wa soko la ndizi Mabonde [pichana Erick Gwakisa]

sauti ya wafanyabiashara 1

Wametoa malalamiko hayo walipokuwa wakizungumza na Chai FM kwa nyakati tofauti wamesema changamoto ya ubofu wa miundombinu ya soko ni ya muda mrefu na kilio chao hakisikilizwi richa ya mamlaka husika kuchukua ushuru wa soko

sauti ya wafanyabiashara 2

mwenyekiti wa soko hilo Ndg. Daniel Mwakobela amekili kuwepo kwa suala hilo na wamesema si geni kwani walishapeleka malalamiko kwa uongozi na kuonekana kutotendewa kazi.

wafanyabishara wakiwa kwenye soko la ndizi Mabonde[picha na Erick Gwakisa]

hata hivyo ameongeza changamoto nyingine wanayokumbana nayo ni ukosefu wa mifereji ya maji inayopelekea wafanyabiashara na magari kushindwa kuingia ndani ya soko kutokana na ubovu wa Barabara

sauti ya Mwenyekiti wa soko Mabonde

Aidha  naye  mwenyekiti wa soko la ndizi kk lililopo kata ya kyimo wilayani Rungwe. Rashidi  Ambakisye amezungumzia juu ya ubovu wa miundombinu na ukosefu wa dampo la kukusanyia taka, na kuiomba serikali kuweza kutatua changamoto hizo.

Ndizi zikiwa juu ya uchafu[picha na Erick Gwakisa]

sauti mwenyekiti soko la kk

kwa upande wake Amani Mwakyeja mjumbe wa kamati ya uongozi wa soko la ndizi  Mabonde ameishukuru mamlaka ya maji Tukuyu  kwa kuziba chemba iliyokuwa inamwaga maji na kuiyomba serikali kushughulikia changamoto hizo.

sauti ya mjumbe wa soko