Chai FM

Recent posts

27 August 2024, 4:13 pm

Mwenge wa uhuru wakagua miradi ya bil.15 Rungwe

Jamii imeshauriwa kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti rafiki ili kukabiliana ma mabadiliko ya tabianchi. RUNGWE-MBEYA Na Sabina Martin Wananchi wilayani Rungwe mkoani Mbeya wametakiwa kujitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi wenye weledi na sifa siku ya uchaguzi wa serikali…

24 August 2024, 12:48 pm

Mwenge kuzindua miradi ya zaidi ya shilingi bilioni 15 Rungwe

Miradi mbamlibali inatarajiwa kuzinduliwa na mwenge wa uhuru katika halmashauri ya wilaya ya Rungwe RUNGWE-MBEYA Na Lennox Mwamakula Wananchi wilayani Rungwe mkoani  Mbeya wameombwa kujitokeza kupokea mwenge wa uhuru unaotarajiwa kungia siku ya tarehe 27 mwezi  huu  na kutembelea miradi…

24 August 2024, 11:48 am

Kamati za kata kuunda timu za ushindi Rungwe

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Issa mwakagenda akiongea kwenye baraza la wazazi la chama cha mapinduzi jamii imeshauriwa kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ili kupata viongozi bora RUNGWE-MBEYA Na lennox Mwamakula Kamati za utekelezaji  za kata zimatakiwa…

20 August 2024, 9:47 am

Ajinyonga baada ya gari yake kupata ajali

Wivu wa mapenzi na tatizo la uchumi imetajwa kuwa chanzo cha watu wengi kufanya mamuzi magumu hata kuondoa uhai wao wenyewe Na Sabina Martin – Rungwe Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Shafki Mkwama amekutwa amejingonga nyumbani kwake kijiji cha…

6 August 2024, 11:56 am

Baraza la madiwani laazimia kuwafuta kazi watumishi Rungwe

Watumishi wa uma wametakiwa kuwa mstari wa mbele kusimamia maadili ya kazi kwa lengo la kuleta ufanisi katika utendaji. RUNGWE-MBEYA Na Lennox Mwamakula Kufuatia halmashauri ya wilaya ya Rungwe kukusanya asilimia 102 ya makusayo ya fedha kwa mapato ya ndani…

4 August 2024, 3:10 pm

Zaidi ya shilingi bilioni 2.9 kujenga kituo jumuishi Rungwe

Zao la parachichi linakwenda kuongezewa thamani baada ya serilikali kujenga kituo cha kuhifadhia mbogamboga na matunda. RUNGWE-MBEYA Na Lennox Mwamakula Mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa kituo jumuishi cha kuongeza thamani ya mazao ya bustani hususani parachichi amekabidhiwa eneo la…

4 August 2024, 1:26 pm

Baraza la madiwani lakemea vitendo vya ulawiti Busokelo

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Jafarr Hanniu akimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Busokeo Bi, Loema Peter [Picha na Lennox Mwamakula] Kutokana na kuwepo kwa vitendo vya ukatili jamii imetakiwa kutoa taarifa kwa vingozi wa serikali ili kuweza kuwabaini…

30 July 2024, 3:47 pm

Elimu kutolewa juu ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto Busokelo

ASP Mstapher akitoa kwa wananchielimu juu ya vitendo ukatili ili kukabiliana na vitendo ya ukatili kwenye jamii jeshi la polisi limeomba ushirikiano ili kuwabaini wanao fanya vitendo hivyo. RUNGWE-MBEYA Na Lennox mwamakula Jamii  imeshauriwa  kutoa  ushirkiano  kwenye jeshi la polisi…

Kuhusu Chai FM

Chai FM radio ni radio inayomilikiwa na Umoja wa wakulima wa Chai Rungwe, Ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha mkulima wa Chai wilaya ya Rungwe anapata taarifa sahihi ambazo zitasaidia kuendeleza zao la Chai pamoja na shughuli zake za kiuchumi, Elimu na Kijamii.

Uwepo wa radio Chai FM umesaidia mkulima wa zao la Chai wilaya ya Rungwe kupata taarifa kwa wakati zinazohusu zao la chai na mwenendo wake pamoja na elimu juu ya kilimo biashara kwa zao la chai na mazao mengine pamoja na ufugaji.

Hii ni kutokana na uguu wa kufikisha taarifa ya masuala ya kilimo kwa wakulima wa chai jiografia ya wilaya ikiwa ni kikwazo kwa wakulima kupata taarifa mbalimbali za ndani na nje ya wilaya pamoja na mpango wa kilimo endelevu.

Dira

Kuona jamii ya wakulima na wafugaji wa wilaya ya Rungwe wanakuwa na maisha bora

Dhamira

Kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Wilaya ya Rungwe kuelimisha na kutoa taarifa za kilimo, mifugo, biashara,viwanda na habari za kijamii kupitia vipindi vya redio.

Chai Fm Radio inasikika maeneo tofauti kama ifuatavyo

Mkoa wa Mbeya – Wilaya za Rungwe, Busokelo, Kyela, na Mbeya Vijijini kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Njombe – Wilaya za Makete, Ludewa

Mkoa wa Songwe – Wilaya za Ileje na Songwe kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Ruvuma – Wilaya za Mbinga na Nyasa.

Lakini pia chai Fm inapatikana ukiwa popote duniani kupitia radiotadio.co.tz/chaifm/