Chai FM
Chai FM
8 May 2023, 8:22 am
RUNGWE Na, Robert Mwakyusa Walimu wilayani Rungwe wameaswa kuwa na mbinu mpya za ufundishaji ili kuboresha ufaulu wa wanafunzi wa masomo ya sayansi. Hayo yamejili kwenye baraza la madiwani lililo fanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa halmashuari ya Busokelo.…
20 December 2022, 11:18 am
KIPINDI: Sikiliza kipindi cha mimi na afya yangu makala maalumu kuhusu Uvumi juu ya chanjo ya Uviko-19 wilayani Rungwe. sikiliza hapa sehemu ya kwanza .
16 December 2022, 12:16 pm
RUNGWE- MBEYA NA JUDITH MWAKIBIBI Kutokana na kukosekana kwa mbolea ya ruzuku kwa baadhi ya maeneo Wilaya Rungwe Mkoani Mbeya wakulima wametakiwa kuwa na subira wakati serikali ikiendelea kulishughulikia suala hilo. Hayo yamebainishwa na afisa kilimo wilayani hapa Bw Juma…
16 December 2022, 12:09 pm
RUNGWE- MBEYA NA: SABINA MARTIN Msimu huu wa mvua zilizoanza kunyesha wilayani Rungwe mkoani Mbeya wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari na kuzingatia afua za afya ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu. Akizungumza na Chai FM ofisini kwake afisa…
16 December 2022, 11:53 am
RUNGWE, Imeelezwa kuwa matumizi ya dawa za binadamu bila kufuata ushauri wa daktari ni chanzo cha usugu wa magonjwa na hatimaye kupelekea kifo. Hayo yamesemwa na mganga mkuu wa Wilaya ya Rungwe Dkt Diokles Ndaiza wakati akizungumza na Chai…
12 October 2022, 4:08 pm
RUNGWE-MBEYA NA: SABINA MARTIN Wazazi na walezi wilayani Rungwe mkoani Mbeya wametakiwa kutenga muda wa kukaa na kuzungumza na watoto wao kuhusu mambo mbali mbali ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili vinavyoendelea katika jamii. Rai hiyo imetolewa na baaadhi ya…
12 October 2022, 3:56 pm
RUNGWE-MBEYA NA:SABINA MARTIN Kuelekea madhimisho ya siku ya mbolea duniani ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo octoba 13 wakulima wilayani hapa wametakiwa kutumia mbolea kwa usahihi ili kupata mazao mengi. Akizungumza kwa njia ya simu na Chai FM afisa kilimo wilayani…
23 September 2022, 5:41 am
RUNGWE-MBEYA NA,JUDITH MWAKIBIBI Kutokana na kampeni inayoendelea ya usalimishaji wa silaha kitaifa wananchi wilayani Rungwe mkoani Mbeya wametakiwa kusalimisha silaha haramu zinazomilikiwa kinyume na utaratibu. Akizungumza katika studio za radio chai FM mrakibu wa jeshi la polisi Wilayanl ya Rungwe…
12 September 2022, 5:26 pm
RUNGWE-MBEYA, NA:LOVENESS RAJABU Wafanyabiashara wa ndizi wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wameeleza bei ya ndizi kwa kipindi hiki cha kiangazi. Wakizungumza na Chai FM wafanyabiashara wa ndizi katika soko la Mabonde wamesema kuwa kwa sasa bei ya ndizi ipo chini…
10 September 2022, 9:26 am
RUNGWE-MBEYA Kupitia TOZO ya miamala ya simu, Serikali imetoa jumla ya shilingi Million 12.5 kwa ajili ya ukamilishaji wa chumba Cha darasa katika shule ya Sekondari Ndembela one iliyopo kata ya Makandana. Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe imetoa kiasi…
Chai FM radio ni radio inayomilikiwa na Umoja wa wakulima wa Chai Rungwe, Ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha mkulima wa Chai wilaya ya Rungwe anapata taarifa sahihi ambazo zitasaidia kuendeleza zao la Chai pamoja na shughuli zake za kiuchumi, Elimu na Kijamii.
Uwepo wa radio Chai FM umesaidia mkulima wa zao la Chai wilaya ya Rungwe kupata taarifa kwa wakati zinazohusu zao la chai na mwenendo wake pamoja na elimu juu ya kilimo biashara kwa zao la chai na mazao mengine pamoja na ufugaji.
Hii ni kutokana na uguu wa kufikisha taarifa ya masuala ya kilimo kwa wakulima wa chai jiografia ya wilaya ikiwa ni kikwazo kwa wakulima kupata taarifa mbalimbali za ndani na nje ya wilaya pamoja na mpango wa kilimo endelevu.
Dira
Kuona jamii ya wakulima na wafugaji wa wilaya ya Rungwe wanakuwa na maisha bora
Dhamira
Kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Wilaya ya Rungwe kuelimisha na kutoa taarifa za kilimo, mifugo, biashara,viwanda na habari za kijamii kupitia vipindi vya redio.
Chai Fm Radio inasikika maeneo tofauti kama ifuatavyo
Mkoa wa Mbeya – Wilaya za Rungwe, Busokelo, Kyela, na Mbeya Vijijini kwa baadhi ya maeneo
Mkoa wa Njombe – Wilaya za Makete, Ludewa
Mkoa wa Songwe – Wilaya za Ileje na Songwe kwa baadhi ya maeneo
Mkoa wa Ruvuma – Wilaya za Mbinga na Nyasa.
Lakini pia chai Fm inapatikana ukiwa popote duniani kupitia radiotadio.co.tz/chaifm/