Chai FM
Chai FM
15 September 2023, 12:58 pm
Jamii inatakiwa kuwalea na kuwalinda watoto yatima katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuwalea katika mazingira yenye usalama kwao. Na Lennox Mwamakula Ili kukabiliana na wimbi la watoto waishio katika mazingira magumu uongozi wa kijiji na kata ya Ndanto…
13 September 2023, 1:16 pm
Wanafunzi wa darasa la saba wanatajia kufanya mitihani kote nchini hivyo jamii imeshauriwa kuwa sehemu ya watoto hao wakati wote ili wanafunzi waweze kufanya vizuri. Na Bahati Obel – Rungwe, Mbeya Wazazi na walezi wilayani Rungwe mkoani Mbeya wametakiwa kuhakikisha…
13 September 2023, 10:45 am
Kutokana na wilaya ya Rungwe kuwa na kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula, biashara, matunda na mbogamboga rai imetolewa kulima pia zao la Strawberry kutokana na zao hilo kustawi wilayani Rungwe mkoani Mbeya. Na Evodier Ngeng’ena – RungweWakulima wilayani Rungwe…
12 September 2023, 1:37 pm
Mimba za utotoni ni miongoni mwa sababu zinazosababisha wasichana wengi kutotimiza ndoto zao huku takwimu zikionesha asilimia 40 ya wasichana huacha masomo kutokana na mimba, hii ni kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2016 wa Human Rights Watch. Frida Mwaipopo…
12 September 2023, 8:11 am
Utamaduni wa watu wengi kutoandika wosia imetajwa kuwa chanzo cha migogoro ya ardhi katika jamii nyingi nchini Tanzania huku mila na desturi zikitajwa. Na Lennox Mwamakula- Rungwe Jamii imeshauriwa kuwa na utaratibu wa kuandika wosia ili kuondokana na mkanganyiko juu…
11 September 2023, 12:00 pm
Kuelekea uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa 2024 vyama vya upinzani wameeleza mbinu watakazozitumia kuking’oa chama tawala madarakani. Na Cleef Mlelwa- Makambako Wananchi wa halmashauri ya mji wa Makambako wametakiwa kuwaondoa madarakani viongozi wote wa kisiasa ambao wameshindwa kutatua changamoto…
8 September 2023, 10:11 am
RUNGWE-MBEYA Na Lennox Mwamakula Mkuu wa wilaya ya Rungwe Jafari Hanniu ametakiwa kusimamia vizuri mradi wa maji wa Ikuti –lyenje ili mradi huo ukamilike kwa muda ulioyo pangwa . Kauli hiyo imetolewa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru…
6 September 2023, 11:39 am
RUNGWE – MBEYA Na Fadhili Mwaifulile Jamii wilayani Rungwe Mkoani Mbeya imetakiwa kusimamia maadili kwa watoto wao hususani watoto wa shule za misingi na sekondari. Kauli hiyo imetolewa na katibu tawala wa wilaya ya Rungwe ndg,ALLY KIUMWA kwenye sherehe za…
6 September 2023, 11:08 am
RUNGWE – Mbeya Wananchi wilayani Rungwe watakiwa kuchangamkia fursa ya uwepo wa mbio za mwenge kuongeza kipato chao. Na Lennox Mwamakula Wananchi Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya Wametakiwa Kujitokeza Kwa Wingi Wakati Mapokezi Ya Mwenge Wa Huru Katika Kijiji Cha Ikuti…
18 August 2023, 12:21 pm
Na Lennox Mwamakula Wananchi wa kata ya Luteba Halmashauri ya Busokelo wameonesha kufurahishwa na ujenzi wa daraja ambalo linaunganisha kata ya Luteba na Lufilyo. Akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Lulasi kata ya Luteba Mbunge wa Jimbo la…
Chai FM radio ni radio inayomilikiwa na Umoja wa wakulima wa Chai Rungwe, Ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha mkulima wa Chai wilaya ya Rungwe anapata taarifa sahihi ambazo zitasaidia kuendeleza zao la Chai pamoja na shughuli zake za kiuchumi, Elimu na Kijamii.
Uwepo wa radio Chai FM umesaidia mkulima wa zao la Chai wilaya ya Rungwe kupata taarifa kwa wakati zinazohusu zao la chai na mwenendo wake pamoja na elimu juu ya kilimo biashara kwa zao la chai na mazao mengine pamoja na ufugaji.
Hii ni kutokana na uguu wa kufikisha taarifa ya masuala ya kilimo kwa wakulima wa chai jiografia ya wilaya ikiwa ni kikwazo kwa wakulima kupata taarifa mbalimbali za ndani na nje ya wilaya pamoja na mpango wa kilimo endelevu.
Dira
Kuona jamii ya wakulima na wafugaji wa wilaya ya Rungwe wanakuwa na maisha bora
Dhamira
Kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Wilaya ya Rungwe kuelimisha na kutoa taarifa za kilimo, mifugo, biashara,viwanda na habari za kijamii kupitia vipindi vya redio.
Chai Fm Radio inasikika maeneo tofauti kama ifuatavyo
Mkoa wa Mbeya – Wilaya za Rungwe, Busokelo, Kyela, na Mbeya Vijijini kwa baadhi ya maeneo
Mkoa wa Njombe – Wilaya za Makete, Ludewa
Mkoa wa Songwe – Wilaya za Ileje na Songwe kwa baadhi ya maeneo
Mkoa wa Ruvuma – Wilaya za Mbinga na Nyasa.
Lakini pia chai Fm inapatikana ukiwa popote duniani kupitia radiotadio.co.tz/chaifm/