Chai FM

Recent posts

1 November 2023, 7:40 pm

Madiwani Rungwe waonywa kuingilia majukumu ya watendaji

Mkurugenzi wa halmashauri ya Busokelo wa pili kutoka kulia akijiandaa kusoma majina ya waliopata tuzo. Kutokana na baadhi ya madiwani kuingilia majukumu ya watendaji wa vijiji, imeelezwa imekuwa sababu ya kutofanya majukumu yao ipasavyo. Na Evodia Ngeng’ena : Rungwe- Mbeya…

30 October 2023, 9:33 am

Rungwe yazindua programu jumuishi kupuguza tatizo la afya ya akili

Matatizo mengi ya afya ya akili ni matokeo ya kutozingatia malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto katika hatua zake za ukuaji kwa kipindi cha kuanzia mwaka 0-8. Na Sabina Martin – Rungwe  Utekelezaji madhubuti wa programu jumuishi ya…

25 October 2023, 10:06 am

Rungwe yakabiliwa na udumavu kwa asilimia 26.5

Ulaji wa chakula usiozingatia lishe bora umetajwa kuwa sababu inayochangia udumavu kwa watoto wengi wilayani Rungwe. Na Lennox Mwamakula, Rungwe Imeelezwa kuwa halmashauri ya wilaya ya Rungwe inakabiliwa na kiwango cha udumavu kwa asilimia 26.5 huku sababu ikitajwa kuwa ni…

16 October 2023, 11:48 am

Wananchi Tukuyu walilia matuta kupunguza ajali za barabarani

Na Sabina Martin Rungwe-MbeyaKufuatia uwepo wa ajali za mara kwa mara katika eneo la ushirika mji mdogo wa Tukuyu wilayani Rungwe mkoani Mbeya wananchi wa eneo hilo wameiomba serikali kuweka matuta katika eneo hilo. Baadhi ya wananchi waliozungumza na chai…

7 October 2023, 8:11 am

Ujio wa vituo vya afya kuwa mkombozi kwa wananchi

kituo cha afya ndanto {picha na lennox mwamakula} wananchi wafurahia huduma ya afya wilaya rungwe kutokana na kuondokana na changamoto ya muda mrefu. RUNGWE-MBEYA Na lennox mwamakula Jumla ya wakazi elfu kumi na nanene wanaenda kunufaika na huduma ya afya …

30 September 2023, 3:04 pm

Taulo zimekuwa mkombozi kwa wanafunzi wa kike mashuleni

wanafunzi wa shule ya sekondari tukuyu wilayani Rungwe wakiwa wanapokea taulo[picha na lennox mwamakula] jamii imetakiwa kuendelea kumsaidia mtoto wa kike ili aweze kuondokana na vikwazo vinavyoweza kumkwamisha kutimiza ndoto zake RUNGWE-MBEYA Na lennox mwamakula Jumla ya pisi elfu ishirini…

21 September 2023, 4:40 pm

Zaidi ya watoto elfu 86 kupata chanjo ya polio Rungwe

Halmashauri ya wilaya ya Rungwe inatarajia kuwafikia watoto zaidi ya elfu themanini na sita na kuwapatia chanjo ya polio ambayo imezinduliwa rasmi hii leo katika mikoa sita yenye hatari ya kupata ugonjwa huo hapa nchini. Na Sabina martin – RungweJamii…

21 September 2023, 4:08 pm

Milioni 362 kujenga stendi ya vumbi Tukuyu mjini

Kukamilika kwa stendi ya vumbi maarufu kama stendi ya Noah Tukuyu mjini itakuwa chachu ya maendeleo kwani itaondoa adha ya watumiaji wa stendi hiyo kwa msimu wa masika na kiangazi. Na Lennox Mwamakula – Rungwe-MbeyaJumla ya shilingi milioni 362 zimetengwa…

20 September 2023, 6:18 pm

Watoto elfu 34 kupatiwa chanjo ya polio halmashauri ya Busokelo.

watoto wenye mahitaji maalum pia wanahaki ya kupata hii chanjo ya polio hivyo msiwafungie ndani wapeni nafasi ya kupata chanjo. Na Sabina Martin – RungweWazazi na walezi katika halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe mkoani Mbeya wametakiwa kutowafungia watoto wenye mahitaji…

Kuhusu Chai FM

Chai FM radio ni radio inayomilikiwa na Umoja wa wakulima wa Chai Rungwe, Ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha mkulima wa Chai wilaya ya Rungwe anapata taarifa sahihi ambazo zitasaidia kuendeleza zao la Chai pamoja na shughuli zake za kiuchumi, Elimu na Kijamii.

Uwepo wa radio Chai FM umesaidia mkulima wa zao la Chai wilaya ya Rungwe kupata taarifa kwa wakati zinazohusu zao la chai na mwenendo wake pamoja na elimu juu ya kilimo biashara kwa zao la chai na mazao mengine pamoja na ufugaji.

Hii ni kutokana na uguu wa kufikisha taarifa ya masuala ya kilimo kwa wakulima wa chai jiografia ya wilaya ikiwa ni kikwazo kwa wakulima kupata taarifa mbalimbali za ndani na nje ya wilaya pamoja na mpango wa kilimo endelevu.

Dira

Kuona jamii ya wakulima na wafugaji wa wilaya ya Rungwe wanakuwa na maisha bora

Dhamira

Kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Wilaya ya Rungwe kuelimisha na kutoa taarifa za kilimo, mifugo, biashara,viwanda na habari za kijamii kupitia vipindi vya redio.

Chai Fm Radio inasikika maeneo tofauti kama ifuatavyo

Mkoa wa Mbeya – Wilaya za Rungwe, Busokelo, Kyela, na Mbeya Vijijini kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Njombe – Wilaya za Makete, Ludewa

Mkoa wa Songwe – Wilaya za Ileje na Songwe kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Ruvuma – Wilaya za Mbinga na Nyasa.

Lakini pia chai Fm inapatikana ukiwa popote duniani kupitia radiotadio.co.tz/chaifm/