Chai FM

Baraza limewafuta kazi watumishi wazembe Rungwe

19 February 2026, 11:15 am

Baadhi ya madiwani wakiwa kwenye kikao cha baraza halmashauri ya wilaya ya Rungwe[picha na Lennox Mwamakula]

watumishi wa uma wanatakiwa kufuata kanuni na sheria za kazi kama zinavyoelezwa ili kuleta matokeo chanya kwa wanao watumikia

Rungwe-Mbeya

Na Lennox Mwamakula

Kikao cha Baraza la madiwani halimashauri ya wilaya ya Rungwe kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2026/2027 na limepitisha bajeti ya shilingi Bilioni 69.3 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.

 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Ndg,Gabriel Mwakagenda amewapongeza watumishi kwa ushirikano wanao uonyesha kwenye usimamiaji wa fedha za miradi zinazo tolewa na serikali kuu amesema fedha zinasimamiwa vizuri na miradi inaonekana

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mh, Gabriel Mwakagenda akitolea ufafanuzi kwenye moja hoja zizizo ibuliwa na madiwani

Sauti ya Mwenyekiti wa halmashauri

Akitoa salamu za serikali mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh,Jaffar Haniu amempongeza mkurugenzi mtendandaji wa halmashauri pamoja na wataam kwa kuanda rasim ya bajeti iliyobeba maono ya wana Rungwe na inaendana na Dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025/2050

sauti ya mkuu wa wilaya 1

Pia Hanniu amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya wazazi na walezi vijana wao kutokuwa na cheti cha kuzaliwa au namba ya Nida kitendo ambacho kinachangia kukosa sifa za kupata ajira,hivyo amewaomba madiwani wawamasishe wannchi kwawena nyaraka hizo muhimu pindi nafasi mbalimbali za ajira zinapo toka vijana wewezi kuzipata

sauti ya mkuu wa wilaya 2

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Rungwe Mh, Anthon Mwantona amewaomba mkurugezi,  watendaji pamoja na madiwani kutafuta mapato ya ndani ili kuweza kuendelea kukamilisha miradi inayotekelezwa kwa wakati

sauti ya Mh,Mwantona

Katika hatua nyingine Baraza hilo la madiwani wilayani Rungwe limeazimia kuwafuta kazi watumishi wa watatu wa halmashauri kwa utolo kazini akitolea ufafanuzi huo wa mazimio hayo Mwenyekiti wa halmashauri Ndg,Gabrie Mwakagenda amesema mbele ya baraza yaliwasilishwa mashauri mnne ambapo amesema shauri moja limerudishwa kwaajila ya kuanza upya utaratibu

Mwakagenda amewasihi watumishi waliopata dhamana ya kuwatumikia wananchi kufauta taratibu,sheria  na miongozo na kanuni za utumishi kama zinavyo elekekezwa

sauti mwenyekiti wa Baraza

Kikao hicho cha baraza la madiwani kimefanyika kwenye ukumbi la halmashauri wa John Mwankenja Tarehe 18/02/2026