Chai FM
Chai FM
8 October 2025, 9:59 pm

jamii imetakiwa kujenga utaratibu wa kutoa taarifa kwenye vyombo ya kisheria kuhusu vitendo vya utatili
MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Vijana nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika suala la kupinga vitendo vya ukatili kwani wao ndiyo nguvu kazi ya Taifa
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Dawati la jinsia na watoto Mkoa ASP Veronica Ponera kwenye kuhitimisha mafunzo kwa vijana,yaliyohusu sanaa na maendeleo ya vijana yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Gr Hotel uliopo soweto mkoani Mbeya amesema kumekwepo na wimbi kubwa la vijana kuto jitambua ambapo kunapelekea vijana kujingiza kwenye vitendo visivyo kubalika kwenye jamii

Hivyo ASP Ponera amewasihi vijana waliopatiwa elimu ya kujitabua ya namna kupinga vitendo vya ukatili waende kuelimisha wengine juu ya matukio ya mbalimbali yakiwemo matukio ya ubakaji,utumiaji wa madawa ya kulevya

Sauti ya mkuu wa dawati la njisia na watoto mkoa wa Mbeya ASP Veronica Ponera
Naye mratibu wa masuala ya vijana mkoa wa Mbeya Ndugu,Francis Ngelela amesema kupitia elimu waliyo ipata vijana wandee kuwa mabarozi kwa wengine waliokosa fursa ya kupata elimu hiyo
Sauti ya Mratibu wa vijana mkoa wa Mbeya Ndugu Francis
Godrich Izack Mgonja ni mkurugenzi wa taasisi kaa kijanja amesema lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo vijana kuwa na uelewa mpana juu ya masuala ya elimu ya afya ya uzazi,namna ya kupinga vitendo vya ukatili kwa kutumia sanaa zao
Sauti ya Mkurugenzi wa Taasisi ya kaa kijanja 1
Aidha mkurugenzi huyo amesema kupitia mafunzo waliopatiwa wakayatumie vizuri kwenye jamii kwakupitia sanaa wataenda kujiboresa kwenye kazi zao wanazozifanya
Sauti ya Mkurugenzi wa Taasisi ya kaa kijanja 2
Kwa upande wao vijana walionufaika na mafunzo hayo wamesema kupitia elimu walioipata wanaenda kutumia kama walivyo fundishwa na kwenda kuibadirisha jamii yenye mitazamo hasi
Sauti za wanufaika