Chai FM

Madai ya wauguzi kufanyiwa kazi kabla ya Mei 31

30 May 2025, 9:49 am

wauguzi wakiwa kwenye maandamano kwenye siku ya kuadhimisha siku ya wauguzi Duniani [picha na Lennox Mwamakula]

Baada ya wauguzi kulalamikiwa madai yao serikali imeamua kushughulikia ili kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa

Na Lennox Mwamakula

Tanzania ikiungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya wauguzi Duniani Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh.Jaffar Hanniu  amewagiza wakurugenzi watendaji wa halmashauri zote za mkoa wa Mbeya na Taasisi zininge zinazo husika na masuala ya afya kushuguliki madai ya wauguzi na wakunga kabla ya mei 31 mwaka 2025.

Maagizo hayo yametolewa na mkuu wa wilaya Rungwe akimwakilisha  mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Mbeya  kwenye maadhimisho ya kusherekea siku ya wauguzi  yaliyo addhimishwa kimkoa katika halmashauri ya Busokelo kwenye viwanja vya shule ya msingi Lwangwa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh,Jaffar Hanniu akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani: Picha na Lennox Mwamakula

Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasim katibu wa  TANNA Bi, Kiliana Tulyanje amesema wauguzi  wameendelea kufanya jidihada mbalimbali kuhakisha jamii ya watanzania inakuwa salama na afya njema

Risala wauguzi

Hata hivyo Bi,Tulyanje amebainisha changamoto wanazo kabiliana nazo wauguzi ikiwa ni pamoja na uhaba wa wauguzi katika halmashauri mbalimbali zilimo ndani ya mkoa wa mbeya  kutokana sera ya nchi na ilani ya chama cha mapinduzi ya kuwa na zahanati kwa kila kijiji

Risala kuhusu changamoto

Hata hivyo wauguzi wametoa mapendekezo kwa serikali kuweka utaratibu wa kuwawezesha wauguzi wanapo kwenda kwenye makongamano mbalimbali na kuziamuru halmashauri kuweka umeme kwenye vituo vyote vyakutolea huduma za afya

Sauti ya wauguzi mapendekezo

Akijibu risala hiyo mkuu wa wilaya ya Rungwe amesema madai yanayo lalamikiwa na wauguzi yafanyiwe kazi kama  yalivyo tolewa na Naibu waziri  wa wizara ya utumishi ilivyotolewa akiwa mkoani Iringa ili wauguzi wandelee kufanya kazi zao bila malalamiko

Sauti ya mkuubwa wilaya

Sambamba na hilo Mh,Hanniu amesema serikali imepokea suala la muundo wa utawala na mapitio ya sera ya afya ili wauguzi watambulike rasmi

Sauti ya mkuubwa wilaya 2