Chai FM
Chai FM
2 March 2025, 2:29 pm

Katibu tawala wa wilaya ya Rungwe Ally Kiumwa akizungumza na wanufaika wa mikopo
serikali ya awamu ya sita imefungua dirisha jipya ya mkopo usiokuwa na riba kwa wanawake,vijana na watuwalemavu
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Halmashauri ya wilaya ya Rungwe imetoa mkopo wenye thamani ya shilingi Million 611 kwa vikundi 60 vya wanawake, Vijana na watu wenye Ulemevu ikiwa ni asilimia kumi ya mapato yake ya ndani.
hafla hiyo ya utoaji wa mikopo imefanyika kwenye ukumbi Halmashauri ya wilaya ya Rungwe wa John Mwankenja
Vikundi hivyo ambavyo vimepatiwa mkopo huo visajiliwa kutoka kata zote 29 zilizopo katika tarafa 3 zinazounda Halmashauri ya wilaya ya Rungwe.
Awali kisoma taarifa ya mbele ya mgeni rasmi Kaimu afisa maenddeleo wilaya ya Rungwe Ndg,Israel Alimwene amesema baada ya kamati mbalimbali kuvipitia vikundi hivyo vitabatiwa fedha baada ya kukidhi vigezo vinavyo hitajika

kaimu afisa maendeleo ya jamii Israel Alimwene akisoma Taarifa mbele ya mgeni Rasmi
sauti ya kaimu afisa maendeleo ya jamii Ndg,Israel Alimwene
Kwa upande kwake kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe CASTORY MAKEULA amseama fedha zilizotolewa kwa wanavikundi zikafanye kazi iliyo kusudiwa

sauti ya kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Rungwe
Naye mgeni rasmi katika hafla Katibu Tawala Wilaya ya Rungwe Bwana Ally Said Kiumwa ambapo pamoja na mambo mengine amewasisitiza wanufaika wa mikopo hii kuendeleza na kukuza bunifu zao ili iwaletee tija na maendeleo ambayo itasaidia kurejesha fedha za serikali kwa wakati
Aidha amevionya vikundi kutothubutu kutumia mikopo kinyume na maelezo ya maombi ya mikopo yao akitolea mifano kama kutumia fedha kwa ajili ya ulevi, kutoa mahari,kamali na mengine mengi.
sauti ya katibu Tawala
Hata hivyo Wananchi ambao wamenufaika na mikopo hii wameishukuru serikali inayoongozwa na Mhe Rais samia_suluhu_hassan kwa kutoa mikopo hii kwani kufanya hivi itasaidia kujiondoa katika makucha ya umasikini.
sauti ya wanavikundi