Chai FM

CRDB yatoa vyeti kuipongeza halmashauri ya Rungwe

31 January 2025, 4:20 pm

Na Sabina Martin – Rungwe

Halmashauri ya wilaya ya Rungwe imepongezwa na Benki ya CRDB kwa ukusanyaji wa mapato pamoja na ufaulu mzuri kwa matokeo ya kidato cha nne na chapili huku ikishika nafasi ya kwanza kwa mkoa wa Mbeya.

Bi. Devotha Kalinga kulia akimkabidhi cheti cha pongezi mwenyekiti wa halmashauri ya Rungwe Mh. Mpokigwa Mwankuga katika ukumbi wa halmashauri ya Rungwe ( picha na Sabina Martin)

Benki ya CRDB kupitia kwa meneja wake Bi. Devotha Kalinga imekabidhi vyeti vya pongezi kwa halmashauri ya Rungwe kwa ukusanyajinmzuri wa mapato pamoja na matokeo mazuri ya mtihani wa kidato cha pili na kidato cha nne.

Akikabidhi vyeti hivyo meneja wa benki ya CRDB tawi la Tukuyu  Bi. Devotha Kalinga amesema kwamba ukusanyaji mzuri wa mapato kwa halmashauri ya Rungwe unachagizwa pia na ushiriki wa Benki hiyo katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika halmashauri ya wilaya ya Rungwe.

Katika hatua nyingine amesema kuwa kiwango kizuri Cha ufaulu katika halmashauri ya Rungwe ni usimamizi na ushirikiano mzuri uliopo baina ya viongozi, walimu, wazazi, wanafunzi pamoja na taasisi mbalimbali.

Sauti ya meneja wa CRDB Rungwe

Vyeti hivyo vimetolewa kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Rungweb Mh. Mpokigwa Mwankuga na Mkurugenzi wa halmashauri ya Rungwe Bw. Renatus Mchau aliyewakilishwa na Kaimu mkurugenzi Bw. Castory Makeula.

Bw. Castory Makeula akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Bi. Devotha Kalinga meneja wa CRDB Rungwe