Chai FM
Chai FM
27 March 2026, 2:52 pm
Baada ya kiwanda cha Wakulima Tea Company kufungwa tangu mwezi wa tano mwaka 2025 sasa wakulima na mwekezaji mwenza wamekuja na mkakati wa kuanza uchakataji wa majani mabichi ya chai katika kiwanda hicho.

Na Sabina Martin – RUNGWE,
Mkutano mkuu maalumu wa chama cha ushirika cha wakulima wadogo wa chai Rungwe na Busokelo RBTCJE wameadhimia kupunguza kilo moja ya majani mabichi ya Chai kutoka shilingi 366 ya awali hadi 256 kwa lengo la kuwezesha kiwanda cha WATCO kujiendesha kwa kipindi cha miezi 12 hadi 15.
Maadhimio hayo yamekuja wakati ambao kiwanda cha wakulima Tea Company ( WATCO) kilisimamisha shughuli zake za uzalishaji kwa kipindi cha mwaka mmoja kutokana na gharama kubwa za uendeshaji zilizosababishia kiwanda hicho hasara, ikiwa ni pamoja na gharama za kifedha zaidi ya Bil. 12.8 kwa kippindi cha miaka mine.
Wakitoa maoni yao baadhi ya wajumbe wwa mkutano huo, wameomba uongozi wa WATCO kutochelewesha malipo ya majani mabichi kwa wakulima punde tu kiwanda hicho kitakapoanza shughuli zake rasmi.
Akijibu swala hilo mwakilishi wa mkutano huo kutoka Wakulima Tea (WATCO) Bw. Petter Luswema amesema kwamba ucheleweshaji wa fedha za mkulima hautojirudia kwani kwasasa wameandaa mfumo maalumu wa kumlipa mkulima kwa kufungua account maalum kwaajili ya malipo hao.
Ally Kiumwa ni katibu Tawala wilaya ya Rungwe akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ametoa rai kwa viongozi wa amcos kutoa elimu kwa wakulima juu ya bei hiyo mpya huku akisisitiza wakulima kuwatumia maafisa ugani waliopo katika maeneo yao katika kilimo cha chai.
Ikumbukwe kwamba maamuzi hayo ya chama cha ushirika cha wakulima wadogo wa chai Rungwe (RBTC-je) ni sehemu ya kuchangia gharama za uanzishwaji wa shughuliza uzalishaji kiwandani kwa kipindi hiki cha mpito kwani wao ni sehemu ya mmiliki wa kiwanda cha Wakulima Tea (WATCO).