Chai FM

Faini ya shilingi laki tatu kutozwa wananchi Rungwe

1 March 2026, 3:50 pm

ni muhimu kila raia kushiriki zoezi la usafi ili kukabiliana magongonjwa

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox mwamakula

Katibu tawala wa wilaya ya Rungwe Bwana Ally said kiumwa amewataka wananchi kujenga utaratibu wa kufanya usafi kwenye makazi yao kila siku ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko

Katibu tawala ametoa  agizo hilo kwenye zoezi la kufanya usafi wa mazingira linalofanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya serikili kuhakikisha kila kaya,taasisi na maeneo mengine ya biashara kuwa na mazingira ya usafi muda wote

Sauti ya katibu twala

Kiumwa amewataka watendaji wa vijiji na kata pamoja na madiwani kuendelea kuwahimiza wananchi kufanya usafi kwenye maeneo yao

Sauti ya katibu tawala  2

Kwa upande afisa mazingira wilaya ya Rungwe Salum kilanga amesema lengo la watumishi kufanya usafi ni kuhamasisha jamii kufanya usafi kwenye maeneo ya makazi pamoja na mahali wanapofanyia shughuli zao za kila siku ili kusaidia kulinda afya ya kila moja

Sauti ya kilanga 1

Aidha kilanga amesema zoezi la ugaguzi kwenye maeneo mbalimbali ya makazi ya watu na sehemu za taasisi  za uma na binafsi litafanyika hivyo mtu au taasisi inatayo shindwa kutekeleza zoezi la ufanyaji wa usafi  sheria kali itachukuliwa ikiwa ni pamoja na kutozwa faini ya shilingi laki tatu.

Sauti ya kilanga 2

Akizungumza kwa niaba ya wananchi  diwani wa kata ya Bulyanga mh, Furaha Mwambungu ameswashukuru watumishi kutoka idara mbalimbali pamoja a wananchi kuichagua kata hiyo kwa mwezi huu kwenda ufanya usafi na kuweka mazingira vizuri

Sauti ya diwani wa kata ya bulyaga

Ikumbukwe kuwa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania imetoa maelekezo ya ufanyaji wa usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi na leo zoez hilo limefanyika kwenye maeneo ya soko la tandale lililopo kata ya bulyaga mji wa Tukuyu