Chai FM

Rungwe iko salama kwa uchaguzi

16 October 2025, 3:07 pm

ikiwa ni takwa la kikatiba wananchi wametakiwa kwenda kuwachagua viongozi wanao wataka siku ya uchaguzi mkuu

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Wito umetolewa kwa wananchi wilayani Rungwe mkoani Mbeya kujitokeza kupiga kura ifikapo octoba 29.2025 kwa wote wenye sifa za kupiga kura.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo octoba 16. 2025 ofisini kwake Mkuu wa wilaya ya Rungwe ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Ndg. Jafar Hanniu amesema wananchi wajitokeze kupiga kura siku hiyo kwani Rungwe ni salama.

Aidha amewataka wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha makundi maaalum ya wanawake wajawazito, wanao nyonyesha,wazee na watu wenye ulemavu kutokaa muda mtrefu kwenye foleni badala yake wapewe kipaumbele.

sauti ya mkuu wa wilaya 1

Katika hatua nyingine ametoa rai kwa wananchi kupuuza taarifa za uchochezi zinazoendelea katika mitandao ya kijamii kwamba siku hiyo hakuna maandamano siku hiyo zaidi ya kupiga kura na kurejea nyumbani.

Sauti ya mkuu wa wilaya 2

Katika hatua nyingine ametoa rai kwa wananchi kutovaa sare za vyama vya siasa siku hiyo ili kuepusha hali ya sintofahamu na uvunjifu wa amani.