Chai FM
Chai FM
23 September 2025, 3:07 pm

kila raia wa Tanzania ana haki ya kupiga kura ya kuchagua kiongozi anaye mtaka kwaajili ya maendeleo
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini imewamba wananchi kushiriki kikamilifu kwenye mikutano ya kampeni inayofanywa na wagombea wa vyama mbalimbali na kwennda kushiriki uchaguzi wa kuchagua Madiwani, Wabunge pamoja na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ifikapo Oktoba 29 mwaka huu kwa amani na utulivu
Kauli hiyo imetolewa na Bi, Amina Talib Ali ambaye ni kamishina wa Tume ya Haki za Binadamu kwenye ukumbi wa mikutano wa jeshi la polisi wilayani Rungwe mkoani Mbeya,kwa dhumuni la kukumbushana katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu
Sauti ya Bi, Amina 1
Bi,Amina amesema Tume ya Haki za Binadamu na utawala Bora inayo jukumu la kulinda haki za binadamu hivyo raia wana haki ya kuwachagua viongozi wao na kuendelea kuhubiri amani ya nchi kwa ndiyo Tunu ya Taifa,hivyo wananchi wanatakiwa kufuta miongozo itakayo wekwa kwenye vituo vya kupigia kura

Sauti ya Bi,Amina 2
Naye Msaidizi wa RPC Mkoa wa Mbeya, SSP Mohamed issa Membe ametoa rai kwa wananchi kuendelea kujitokeza kwenye mikutano ya kampeni ya wagombea wa vyama vyote na kusikiliza sera za vyama vyao na kuwaomba wagombea wasisitize amani na usalama wa nchi kwani hivyo ndiyo kipao mbele kwani amesema bila kuwa na usalama na amani hatuwezi kuwa na uchaguzi
Sauti ya SSP Magembe
Baadhi ya maafisa wa polisi walioshiriki kwenye hafla hiyo ya kujengeana uwezo wamesema jukumu la jeshi la polisi kulinda raia hivyo katika kipindi hiki cha kampeni na baada ya kampeni wataendelea kulinda amani kwenye mikutano
Kwa upande wake askari polisi SGT Fadhili Athuman ameishukuru Tume ya haki za Binaddamu na utawala Bora kwakuwakubusha masuala mbalimbali kuhusu haki za Binadamu na kwenda kuyafanyia kazi yale yote waliyo tolewa na Tume.

Sauti ya Afande Fadhili
Vaileth Maziku ni moja wa maafisa wa polisi walio patiwa elimu kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu amesema wao kama polisi ni wadau muhimu wa ofisi ya Tume ya haki za binadamu kwani jeshi la polisi wanazingatia haki kutokana jamii wanayohidumia
Sauti ya Afande Vaileth
Ikumbukwe kuwa Tume ya haki za binadamu na utawala Bora nchini inaendelea kuwa kumbusha wadau mbalimbali wakiwemo wanahabari na kutumia kalamu zao vizuri juu ya masuala ya haki na utawala bora na wananchi kuwa msitari wa mbele kulinda amani ya nchi katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu