Chai FM
Chai FM
10 September 2025, 4:16 pm

Siku ya kuzuia kujiua duniani inaadhimishwa Kila ifikapo septemba 10. Kila Mwaka ikiangazia Tatizo la afya kwa umma licha ya kuzuilika husababisha vifo vya zaidi ya watu lakini saba kwa mwaka.
Na Sabina Martin
Wakati dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya kuzuia kujiua leo septemba 10. 2025 jamii wilayani Rungwe mkoani Mbeya imetakiwa kukubaliana na hali halisi ya maisha yao badala ya kutaka kukubalika na kila mtu kwenye jamii.
Hayo yanajiri wakati ambapo ikielezwa kwamba watu wengi wanaojiua hukabiliana na msongo wa mawazo unaotokana na hali ngumu ya maisha pamoja na mahusiano huku wahanga wakubwa wakitajwa kuwa ni kundi la vijana.
Akizungumza na Chai FM radio mapema leo katika kipindi cha amka na Chai FM mtaalamu wa saikolojia na jamii Mwl. Kotasi Mbwilo amesema kwamba watu wengi wanafikia maamuzi ya kujiua kutokana na mfadhaiko wa moyo kutokana na hali ya maisha.
Hata hivyo ametoa rai kwa jamii kuwatia moyo na kubadilisha hisia za wale wanaoonekana kujitenga kutokana na msongo wa mawazo.
Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani WHO za mwezi march mwaka 2025 kulikua na visa vya kujiua 720,000 ambapo wanaume wanaongoza mara mbili zaidi ya wanawake katika matukio hayo huku kundi la vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15 – 29 ni asilimia 73 ya vifo hivyo.