Chai FM
Chai FM
10 September 2025, 11:25 am
Baada ya utendaji mzuri wa miaka mitano wana ileje bado wanaimani na Kasekenya

Na Sabina Martin
Tanzania ikiwa inajianda na uchaguzi mkuu oktoba 29 Mwaka huu kampeni zinaendelea katika maeneo tofauti nchini ambapo mgombea ubunge jimbo la ileje kupitia chama cha mapinduzu [CCM] Eng, Godfrey Kasekenya amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kuwachagua wagombea wa nafasi mbalimbali wa chama hicho.
Eng. Kasekenya amewakumbusha wananchi wa jimbo la Ileje baadhi ya miradi inayoendelea kutekelezwa katika jimbo hilo kuwa ni pamoja na Ujenzi wa barabara ya Isongole – Isoko pamoja na Barabara ya Ibungu – Kyimo.

Aidha amesema kwamba katika ilani ya uchaguzi ya 2025-2030 maelekezo katika miundombinu ni kujenga barabara za vijijini ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo.
Somoka kibona, Gaweni amanyisye na Susha Mwampamba ni baadhi ya wananchi waliohudhuria kampeni hizo wameeleza namna Mbunge huyo alivyoifungua wilaya ya ileje kuiunganisha na wilaya zingine kupitia miradi ya barabara huku wakitarajia makubwa zaidi kutoka kwake baada ya uchaguzi.
Akizungumza kwa niaba ya Machifu wa Ileje Chifu Mwampashi ametoa baraka kwa wagombea wote wa chama cha Mapinduzi katika jimbo hilo huku akisisitiza amani na mshikamano miongoni mwa wananchi.
Uzinduzi wa kampeni katika Jimbo la Ileje zimezinduliwa jana septemba 8.2025 katika uwanja wa Itula kata ya Lubanda wilayani Leje mkoani Songwe huku wageni mbalimbali wa chama mkoa wa Songwe wakihudhuria.