Chai FM
Chai FM
8 June 2025, 11:26 am

Ndugu Aliko Mwaiteleke akizungumza na vyombo vya habari {picha na Lennox Mwamakula}
katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu watu mbalimbali wameanda kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Ikiwa Tanzania ikielekea kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu Mdau wa maendeleo wilayani Rungwe mkoani Mbeya ambaye pia ni mkurugenzi wa taasisi ya Mwaiteleke Foundation ndg Aliko Anyambilile Mwaiteleke ametangaza nia ya kugombea ubunge kwenye jimbo la Rungwe kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi {CCM}
Ametoa kauli hiyo akiwa anazungumza na vyombo vya habari kwenye mkutano maalum uliyofanyika mji mdogo wa katumba kata ya Ibhigi Mwaiteleke amesema zoezi la uchukuaji wa fomu pindi chama kitakapo toa ridhaa naye atakuwa ni sehemu ya wagombea kwa mwaka huu
Sauti ya Mwaiteleke 1
Aidha Mwaiteleke ameongeza kuwa muda ukifika atazungunza mengi kuhusu nini anakwenda kuwafanyia wana Rungwe
Sauti ya Mwaiteleke
Ikumbukwe kuwa uchaguzi mkuu ufanyika kila baada ya miaka mitano ya kuwapata madiwani,wabunge na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania