Chai FM

Bonde la ziwa Nyasa hawapoi

2 June 2025, 1:37 pm

Sehemu ya chanzo Cha maji katondo kiilicho vamiwa na wananchi: picha na Sabina Mmartin

Ni jukumu la kila mtu kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji kwani hakuna mtu anayeweza ishi bila maji.

Na Sabina Martin

Wenyeviti wa vijiji na vitongoji wametajwa kuwa chanzo cha wananchi wengi kufanya shughuli za ibinadamu ndani ya mita sitini kutoka katika vyanzo vya maji.

Madai hayo yamekuja kufuatia baadhi ya wenyeviti wa vijiji na vitongoji kujihusisha na uuzaji wa maeneo ya vyanzo vya maji kwa wageni wanaofika katika maeneo yao wakishirikiana na wenyeji wa maeneo hayo.

Hayo yameibuka katika mkutano wa kijiji cha Ibula uliofanyika katika kitongoji cha Kibumbe wenye lengo la kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira na ushirikishwaji wa wananchi juu ya uwepo wa alama za uhifadhi wa chanzo cha maji Katondo zoezi lililo endeshwa na bodi ya maji Bonde la ziwa Nyasa kwa kushirikiana na wataalam mbalimbali wa halmashauri ya Rungwe.

Sauti za wananchi Kiwira

Awali akitoa elimu afisa maendeleo ya jamii kutoka ofisi ya maji bonde la ziwa nyasa Bi. Chiwaya Nkomola ametoa rai kwa viongozi hao kutojihusisha katika mauziano ya maeneo yaliyo ndani ya mita sitini kutoka katika vyanzo vya maji kwani maeneo hayo hayamilikiwi na mtu binafsi.

Aidha amesema kwamba ofisi ya maji bonde la ziwa nyasa mbali na mambo mengine inafanya shughuliza kutunza, kuhifadhi, kuvilinda na kuviendeleza vyanzo vya maji, kutoa elimu kwa wananchi dhidi ya utunzaji wa mazingira.

Sauti ya Bi. Chiwaya afisa maendeleo Bonde la ziwa nyasa

Hata hivyo Bw. Pio Ngobile ambaye ni mpimaji msaidizi wa ardhi halmashauri ya Rungwe ametoa rai kwa wananchi kufika ofisi za ardhi ili kujiridhisha na maeneo wanayotaka kununua ili kuepusha migogoro ya ardhi.

Sauti ya afisa ardhi halmashauri ya Rungwe

Michael Simon Mwamwimbe ni diwani wa kata ya kiwira katika mkutano huo amesema kwamba suala la maendeleo ni jamba mtambuka hivyo wananchi wawe na utayari wa kupokea elimu ya utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji.

Sauti ya diwani kata ya kiwira

Ofisi ya maji bonde la ziwa nyasa imekuwa na utaratibu wa kushirikisha wananchi shughuli mbalimbali za bonde ikiwa ni pamoja na elimu ya kutunza, kulinda na kuviendeleza vyanzo vya maji, pamoja na kuelimisha umuhimu wa uwekaji wa mipaka katika maeneo yaliyoainishwa.

Baadhi ya wananchi wa kijji Cha Ibula wakifatillia elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji: Picha na Sabina Martin

Katika kata ya kiwira mbali na chanzo cha mto katalalifu mipaka itawekwa pia katika chanzo cha katondoKama kwa habari zaidi kuhusu chanzo cha katalalifu bofya hapa na kuhusu chanzo cha mto nyelele bofya hapa, na kujua zaidi kuhusu bonde la ziwa nyasa bofya hapa.