Chai FM

Miaka 20 ya mapambano dhidi ya Usubi tumefika?

26 May 2025, 1:08 pm

washiriki wa mkutano wa wadau wa afya wa Rungwe,Kyela na Ileje katika picha ya pamoja: picha na Lennox Mwamakula

Mapambano dhidi ya ugonjwa wa usubi katika wilaya za Rungwe, Kyela na Ileje yaliyodumu kwa kipindi cha miaka ishirini sasa yamezaa matunda kwa kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.

Na Sabina Martin

Serikali kupitia wizara ya afya kwashirikiana na Taasisi ya Taifa ya utafiti wa magonjwa ya Binadamu NIMR imeombwa kuendelea kufanya utafiti wa ugonjwa wa usubi.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya kyela Mh,Katule Kingamkono kwenye kikao cha siku ya ufunguzi wa hamasa  ya uwasilishaji wa matokeo ya utafiti wa Tathimini ya mambukizi ya ugonjwa wa usubi kilichofanyika kwenye ukumbi wa songwe view resort uliopo boda kyela.

Daktari Akili Kalinga ameeleza kwamba serikali kupitia taasisi ya Taifa ya utafiti wa magonjwa ya Binadamu NIMR imeleta afua mbalimbali kwa ajili ya kupambana na maradhi hayo, huku akisema afua kuu iliyo tekelezwa na program ya wizara ya afya ilikuwa ni kugawa na kumezesha wananchi wote kinga tiba ya Ivermectin tangu mwaka 2000.

Sauti ya Dk. Kalinga kutoka NIMR

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kyela Katule Kingamkono  amesema kutonana na kuwepo kwa viashiria vya ugonjwa huo wa usubi kwenye maeneo ya wilaya za kyela,ileje na Rungwe ameiomba Taasisi ya Taifa ya utafiti wa magonjwa ya Binadamu kuendelea kufanya utafiti wa kina ili kuokoa afya za wananchi.

Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya Kyela

Akitoa neno la shukrani Afisa Tarafa ya Ntebela Noreen  Mwanjela ameishukuru NIMR kwa kufanya tafiti  na kuendelea kuwamezesha dawa watoto ili kutokomeza ugonjwa huo wa usubi kwenye jamii.

Sauti ya afisa tarafa Bi. Noreen

Sambamba na hayo kikao kicho cha hamasa ya uwasilishaji matokeo ya utafiti wa tathmini ya mambukizi ya ugonjwa wa usubi kimewakutanisha watalaam wa afya,maafisa watendaji wa kata,maafisa tarafa,madiwani pamoja na mwakilishi wa neneja wa mpango wa Taifa wa kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaombale na wizara ya afya.