Chai FM
Chai FM
16 May 2025, 10:18 am

ili kukabiliana na vitendo vya ukatili nchini jamii imetakiwa kuwa mstari wa mbele kupinga vitendo hivyo
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Wanaofanyiwa vitendo vya ukatili kwenye jamii wanatakiwa kujenga utaratibu wa kutoa taarifa kwenye vyombo vya kisheria ili waweze kupatiwa msaada wa kisheria.
Kauli hiyo imetolewa na Bupe Suka Polisi kata ya Mpuguso kwenye tamasha la michezo lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la DSW lililofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mpuguso iliyop kijiji cha Mpuguso kata ya Mpuguso amesema vitendo vya ukatili vinaweza kukomeshwa iwapo jamii itaendelea kujenga utamaduni wa kutoa taarifa na kuelimisha juu ya ukatili.

Sauti ya polis kata
Beata Mahenge ni afisa maendeleo kata ya Mpuguso amesema kuwepo kwa matamasha hayo ya kutoa elimu juu ya vitendo vya ukatili na elimu ya afya ya uzazi imesaidia kupunguza vitendo hivyo vya ukatili kwenye kata hiyo kwa kiasi kikubwa.
Sauti ya afisa maendeleo ya jamii
Naye Athuman ni muuguzi kwenye kituo cha afya Mpuguso ametoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana ambapo amewasii vijana na jamii kwa ujumla kuwa na utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara ilikuwa na afya Bora.

Sauti ya muuguzi
Baada ya kupatiwa elimi hiyo baadhi ya vijana wamesema elimu ya afya ya uzazi waliopatiwa wanakuenda kuwa mabalozi kwa vijana wengine
Sauti ya wanufaika
Victor Mwaipungu ni vijana kutoka kikundi cha Mpuguso youth club ambaye ni miongoni mwalio elimu ya afya ya uzazi na kupinga vitendo vya ukatili wameshukuru shirika la DSW kwa kuwajengea uwezo na kuwa mabalozi kwa vijana wengine.
Sauti ya vijana
Mariam Abraham ni mratibu kutoka shirika la DSW amesema wanaandaa matamasha mbalimbali kwenye kata zilizopitiwa na mradi kwa lengo la kushirikiana na serikali kuhakikisha vitendo vya ukatili vinatokomezwa kwenye jamii.
sauti ya mratibu
Sambamba na hilo mratibu amesema ndani ya wilaya ya Rungwe mradi huo unatekelezwa kwenye kata kumi ana ametoa rai kuwa watu waliofika kwenye tamasha hilo kuwa elimu walioipata waweze kuisambaza kwenye jamii
Sauti ya mratibu 2