Chai FM
Chai FM
16 May 2025, 9:51 am

serikali kupitia wizara ya kilimo imekuja na mpango wa kusaidia amccos nchini
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Mbunge wa viti maalum mkoa wa mbeya mh, Sophia Mwakagenda ameishukuru serikali kupitia wizara ya kilimo kwa kujenga Packhouse wilayani Rungwe mkoani Mbeya ili mkulima wa zao Parachichi aweze kupata soko la uwakika baada ya kuvuna
Ametoa kauli hiyo Mbele ya mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa nafaka na mazao mchanyiko [COPRA] Irene Mlola kwenye ukumbi wa ofisi za Amcos ya UWAMARU zilizopo kata ya kyimo wiliyani Rungwe ambapo Mh, Mwakagenda amesema kwaniaba ya wakulima wa parachichi wanashukuru wizara ya kilimo kwa kuwaondolea madalaili kwa hao ndiyo wanao waumiza wakulima na kujinufaisha wao

Sauti ya Mh, Mwakagenda 1
Hata hivyo Mh, Mwakagenda amewaomba mkurugenzi wa COPRA kuboresha Barabara zinazotoka kwenye mshamba ili mkulima aweze kusafirisha mazao kwa urahisi,
Sauti ya Mh, mwakagenda 2
Dadi Sanga ni mkulima na mwanacha wa UWAMARUameiomba serikali kuweka mazingira mazuri ya kusafirisha parachichi kwa kupitia Bandari ya Dar es salaam na Tanga ili tusiendele kutengemea Bandari za nchi jirani

Sauti ya mkulima
Naye Alfred Mwakasangula ni mjumbe wa Bodi ya umoja wa wakulima hao amemshukuru mbunge Sophia Mwakagenda kwa kuwakutanisha na Waziri wa kilimo nchini na amewaomba wakulima wenzake kujituma katika uzalishaji ili jitihata zinazofanywa na serikali ya kuwasaidia ziwe zenye tija
Sauti ya mjumbe
Aidha Mwenyekiti wa UWAMARU ndg,Edward Kabuje amesema lengo ya wizara kufika Rungwe ni baada ya kupeleka kilio chao hivyo Mamlaka ya udhibiti wa nafaka na mazao mchanganyiko imeona kunahaja ya kufika na kukutana na wakulima wa parachichi na kuwapatia elimu ya nmna ya uwendeshaji wa kilimo
Sauti ya Mwenyekiti