Chai FM
Chai FM
11 May 2025, 3:47 pm

wanawake wametakiwa kutumia furusa zilizopo kwenye maeneo yao ili kujikwamua kiuchumi
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Richa ya serikali kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake ,vijana na watu wenyeulemavu mkurugenzi wa Taasisi isiyo kuwa ya kiserikali ya SHE CAN FOUNDATION na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya Mh, Sophia Mwakagenda amesema kuna haja ya kuwepo kwa makongamano mbalimbali ngazi ya kata ya kuwajengea uwezo wanawake nanma ya kupata mikopo ya serikali
Ametoa kauli hiyo kwenye hafla ya kusherekea mafanikio yaliyo patikana ndani ya taasisi ya SHE CAN FOUNDATION iliyotimia miaka kumi tangu kuanzishwa kwake na shehere hizo zimefanyika kwenye wa kivanga top garden uliopo kata ya kyimo

Awali kitoa taarifa fupi ya mafanikio ya taasisi hiyo mratibu ndugu, Abraham Nzunda amesema lengo la kuazishwa kwa taasisi hiyo ni kuwasaidia wanawake waishio kwenye mazingira magumu na kwa muda wa kipindi cha miaka mitano ndani ya halmashauuri ya Rungwe zaidi ya wanawake na wasichana 586 wamefikiwa na kuhudumiwa
sauti ya mratibu wa Taasisi ya SHE CAn FOUNDATION
Naye Mtaala wa masuala ya Saiklojia Mwalimu Kotasi Mbwilo ametoa elimu juu ya masuala ya ndoa na amesema kumekuwepo na wimbi kubwa la wanawake kulaumiwa kwenye jamii kutokana na wanawake wengi kukita sana kwenye utafutaji wa hela kuliko kuhudumia waume zao
Sauti ya Mbwilo
Kwa upande wake mkurugenzi wa Taasisi hiyo Sophia Mwakagenda amesema kuna haja ya kukutana mara kwa mara na wakina mama kwenye maeneo yao ili kuweza kulimishwa namna ya ujazaji wa fomu za mikopo inayotolewa na serikali ili kila mlengwa wa mkopo huo aweze kunufaika

sauti ya mkurugenzi mwakagenda 1
Aidha nao baadhi ya wakulima wa zao la chai wamesema kwa sasa zao hilo halina tija kwao kwani hawajalipwa fedha zao kwa muda wa miezi minne
sauti ya wananchi
Mwakagenda amesema kuhusu suala wakulima wa chai kutolipwa fedha wanazo dai ndani ya mwezi huu wa tano kama wabunge watafuatilia ili kila mkulima aweze kulipwa
sauti ya mwakagenda 2
Sambamba la hilo Mwakagenda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Samia suluhu Hassan kwakuendelea kuwatumikia watanzania kwa kupeleka miradi mbalimbali na kutekelezwa kwa asilimia miamoja na kwa kipindi kifupi cha miaka minne na wanachi kufurahia huduma hizo.