Chai FM
Chai FM
6 May 2025, 5:21 pm

Kwa kutambua kazi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jamii imeendelea kuungana na Dkt,samia kuendelea kuwatumikia wananchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo
RUNGWE – MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Mkuu wawilaya ya Rungwe Mh,Jaffar Hanniu amepokea kiasi ccha shilingi Milioni 1,132,200 kutoka kwenye kikundi cha Mwanamke shujaa kilichopo Tukuyu mjini zikiwa ni fedha kwaajili ya kuchangia Mhesshimiwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hasani ili aweze kuchukua fomu kwaajili ya kugombea Urahis mwaka huu 2025
Zoezi hilo la kupokea fedha hizo limefanyika kwenye ofisi za mkuu wa wilaya ya Rungwe zilizopo Tukuyu Mjini mapema leo Mei 6/ 2025

Akikabidhi kwaniaba ya kikundi Mwenyekiti wa kikundi hicho Bi,Greda Mwakabumbe amesema wazzo la kumchangia Mh, Rais liliasisiwa kwenye siku ya Mwanamke Duniani ambapo wana kikundi walianza kuchangia kidogokidogo mpaka kifikisha kiwango kicho cha fedha
Sauti ya Mwenyekiti 1
Bi,Mwakabumbe ameongeza kuwa wanakikundi wamefikia uwamuzi huo baada ya kuridhika na kazi ya kuboresha miundombinu ya Elimu,Aafya,Maji na barabara kwa kiwango kikubwa
Sauti ya Mwenyekiti 2
Kwa upande wake katibu wa kikundi hicho cha M wanawake Shujaa Mwalimu Elizabert Sekile kililicho wasukuma sana ni namna rais Samia anavyo watumikia watanzania kwa moyo wote
Sauti ya sekile
Akipokea fedha hizo Mh, Hanniu amewashukuru wana kikundi hicho kwakuonyesha moyo wa kizalendo kwa taifa na kutambua kazi zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri wa muungano wa Tanzania wa kuwatumikia wananchi wake
Sauti ya Mkuu wa wilaya Rungwe