Chai FM
Chai FM
28 April 2025, 4:28 pm

Kwenye kikao cha wadau wa Parachichi kilichofanyika hivi karibuni mkoani Dodoma bei itapangwa na wizara na sio Halmashauri.bei itakuwa moja kwa nchi nzima
Na Lennox Mwamakula
Ili kukabiliana na kilio cha wakulima wa zao la parachichi wilayani Rungwe mkoani Mbeya serikali kupitia wizara ya kilimo imekuja na mpango maalum wa kupatia mkulima mbolea ya ruzuku ili aweze kuzalisha parachichi lenye ubora.
Kauli hiyo imetolewa na mbunge wa viti maalumuu mkoa wa mbeya Mhesimiwa Sophia Mwakagenda alipokuwa akizungumza na wananchi wa wilaya ya Rungwe kwenye mkutano wa adhara uliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Bulyaga iliyopo katikati ya mji wa Tukuyu.
Mbunge Mwakagenda amesema kwenye kikao cha wadau wa Parachichi kilichofanyika hivi karibuni mkoani Dodoma bei itapangwa na wizara na sio Halmashauri.bei itakuwa moja kwa nchi nzima, mbolea itatolewa kwa wakulima na hakutakuwa na reject parachichi zitawekwa kwa grade na kuhusu Masoko serikali itaweka nguvu ya kutafuta masosoko ya zao hilo

Kwa upande wao wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wamemuomba mbunge huyo kuwatatulia changamoto ya miundombinu ya barabara ikiwemo barabara ya kutoka Ibungila hadi Tukuyu mjini kwani kipindi cha mvua wananchi wanatumia zaidi ya kiasi cha shilingi elfu kumi na tano kutokana babara kuwa na mashimo
Aidha naye wanchi Jacob Mwambelo amemuomba mbunge kuwakutanisha na madiwani wote kabla ya muda wao kumalizika ili wananchi waweze kujua ni kwanini bei ya maziwa imekuwa chini kuliko bei ya maji na mikakati yao ikoje ili mfugaji aweze kunufaika na anacho zalisha

Hata hivyo Mwakagenda amesema kero hizo za wananchi amezichukua na atashirikiana na Mbunge wa jimbo ili kuweza kuzitatua, Sambamba na hilo Mbunge huyo amekishukuru chama cha Democrasia na maendeleo[CHADEMA] kwa kumlea vizuri kisiasa na amesema ifikapo tarehe 27 june, 2025 baada ya Bunge la jamhuri ya muungano kuvunjwa atajiunga na chama cha mapinduzi [CCM]