Chai FM

Vilio vyatawala kwa wafanyabiashara Rungwe

28 March 2025, 8:32 am

Watumiaji wa vyakula wameziomba mamlaka kuona nmna ya kukabiliana na bei za mazao ya vyakula

RUNGWE –MBEYA

Na Bertha Izengo

Katika msimu huu wa mfungo wa Eid el Fitr Wafanyabiashara  wilayani Rungwe mkoani Mbeya waeleza changamoto  upatikanaji wa bidhaa kwenye maeneo mbalimbali katika kipindi hiki.

 Mmoja wa wafanyabiashara soko la nafaka Tandale Bi.Edina Sanga akizungumza na kituo hiki amesema akiwa muuzaji wa nafaka kama vile karanga bei imepanda ukilinganisha na kipindi cha nyuma kabla ya mfungo.

Sauti ya mfanyabiashara1

Naye Ndg.  Derrick Mkivuyo amegusia katika upandaji wa bei za mchele kipindi hiki cha mfungo,kwani bei za mchele kwa sasa  ametaja kuwa zipo juu na kuomba wakulima kupunguza bei  kwani inawaathiri wafanyabiashara na watumiaji .

Sauti ya mfanyabiashara 2

Naye Ndg. Aselwisye Mvela amesema kuna baadhi ya vyakula vimepanda bei kutokana na kutopatikana kwa urahisi hivyo amewaomba watumiaji kukubaliana na hali

sauti ya mfanyabiashara3

Sambamba na hayo baadhi yao wamesema katika kipindi hiki cha mfungo watu wengi hasa wafanyabiashara wanainuka kiuchumi kutokana na mazingira yalivyo

sauti ya mnunuzi