Chai FM
Chai FM
2 March 2025, 11:55 am

Afisa uthibiti ubora wa shule Halmashauri ya Busokelo Bi,Asha Kibiki akiwa ofisini kweke [picha na Peter Tungu]
katika kwendana na mabadiliko ya sanyasi na teknolojia jamii imetakiwa kuendana na mabadiliko hayo ili kuweza kuanda watoto kuweza kujiajili
BUSOKELO- MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Wadau wa elimu nchini wametakiwa kutumia fursa za uwekezaji zilizopo katika maeneo mbalimbali ili kupanua wingo mpana wa elimu kwa jamii
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa idara ya uthibiti ubora ya shule wilaya ya Busokelo Bi,ASHA KIBIKI kwenye kipindi cha Amka na chaifm amesema kutokana na uwepo wa ardhi ya kuosha wadau waende kwenye halmashauri hiyo kwani kuna uhitaji mkubwa wa shule kutokana na wazazi na walezi kutaka kuona shule za amali zinakuwepo ndani Busokelo ili kuwaondolea adhaa ya kutafuta shule hizo kwenye halmashauri za jirani

Wathibiti ubora wa shule kutoka idara ya elimu wilaya ya Bbusokelo wakitoa elimu kuhusu mtaala mpya wa elimu kwa njia ya redio [Picha na Peter Tungu]
Sauti ya Mkuu wa idara uthibiti ubora wa shule wilaya ya Busokelo Bi,Asha kibiki
Kwa upande wake AMOS KALOLO afisa mthibiti ubora washule halmashauri ya Busokelo amebainisha masomo atakayo soma mwanafunzi kwa shule za msingi

Sauti ya mthibiti ubora shule Mwalimu Amos kalolo 1
Hata hivyo amesema uwepo wa wa mtaala mpya unamwanda mtoto amweze kujiajili pindi atakapo hitimu masomo yake hivyo wazazi na walezi waache tabia ya kuwachagulia masomo watoto kwani wanasabisha kufifisha ndoto za wazo
Sauti ya mthibiti ubora shule Mwalimu Amos kalolo 2
Naye mwalimu Maria Msambule amewaomba wazazi kuwa na tabia ya kufuatilia watoto tangu wakiwa wadogo ili kuweza kutambua kipaji chake
sauti ya mwalimu Maria Msambule