Chai FM

CCM yazidi kuvunja ngome ya CHADEMA Rungwe

11 November 2024, 1:10 pm

Katika kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa chama cha mapinduzi wilayani Rungwe kimezidi kuvuna wanachama wapya kutoka chama kikuu cha upinzani

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Rungwe akizungumza na wanchi wa kata ya Ndanto

Mwenyekiti wa chama cha Mapindizi mkoa wa Mbeya Patrick Mwalunenge  ameviomba vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua za kisheria Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzisheria watu wote wanao tishia usalama wa raia nchini

Mwalunenge ametoa kauli hiyo kwenye viwanja vya ofisi ndogo  za chama cha mapinduzi  tawi la Ntokela kata ya Ndanto wakati wa hafla ya kuwapokea wanachama wapya kutoka chama cha Demokrasia na maendeleo [ CHADEMA] waliojiunga na chama cha mapinduzi

Miongoni mwa wanachama wapya walio jiunga na chama cha Mapinduzi ni aliye kuwa Katibu mwenezi wa chama cha Demokrsia na Maendeleo CHADEMA kata ya Ndanto Ndugu , Aliko Mwanjalila na wanachama wengine ambapo katibu wa chama cha mapinduzi  wilaya Rungwe Abdallal Mpokwa  amesema amefurahishwa na ketendo cha wanachama huyo kurudi ndani ya chama cha mapinduzi

Wanachama wapya waliojiunga na chama cha mapinduzi akila kiapo mbele ya Mwenyekiti wa chama hicho

sauti ya katibu wa chama wilaya ya Rungwe Abdallal Mpokwa

Kwa upande wake aliyekuwa katibu mwenezi wa chama cha demokrasia na maendeleo[ CHADEMA] kata ya ndanto Aliko Mwanjalila amesema ameamua kujiunga na chama cha mapinduzi kutokana na mazuri yanayofanywa na chama hicho na ameshwangazwa na baadhi ya watu kumtishia uhai wake baadaya kutangaza kuhamia chama cha mapinduzi

sauti ya aliko Mwajalila 1

Aidha Mwajalila amewaomba viongozi wa chama cha mapinduzi kumtuma kufanya kazi za chama kwani amesema yupo kwaajili ya kuwa tumikia wana Ndanto na watanzania kwaujumla

sauti ya aliko Mwanjalila 2

Naye Mwenyekiti wa Halmahauri ya wilaya ya Rungwe Mpokigwa Mwankuga  ambaye pia ni mlezi wa kata ya ndanto amesema vipo viashilia vya kuwatishia wanachama wapya wanaojiunga na chama cha mapinduzi hiyo amemuomba Mwenyekiti wa cha mkoa kulichukulia suala hilo kwa ukaribu na kuweza kulifanyia kazi

sauti ya Mwenyekiti wa halmshauri

Akizungumzia sula la uvunjifu wa amani kwenye kata hiyo ya ndando Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa mbeya Patrick Mwalunenge amewaomba viongozi wa dini kuendelea kukemia maovu yaliyomo ndani ya mioyo ya baadhi ya watu wasiyo itakia mema nchi na kuwakumbusha wazazi na walezi kuwakanya watoto wao wasijihusishe na vitendo jivyo vya kuvuruga amani tuliyo nayo bali vijana wajikite katika shuguli za kujingizia kipato,

sauti ya mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa