Viongozi wa serikali za mitaa chachu ya maendeleo Busokelo
7 November 2024, 10:56 am
wanachi wametakiwa kujitokeza kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kwani ni haki yao kuchagua viongozi wanao wataka
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Katika kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenda kwenye vituo vya kupigia kura ili kuchagua viongozi watakao watumikia.
Kauli hiyo imetolewa na katibu tawala wilaya ya Rungwe Ndg Ally Kiumwa kwenye kikao cha Baraza la madiwani la Halmashauri ya Busokelo kilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.ambapo katibu tawala huyo wamepongeza wataamu wa idara,viongozi wa dini pamoja na madiwani kwa kuwahamasisha wananchi kwenda kujiandikisha kwenye daftari la mkazi
sauti ya ally kiumwa 1
Hata hivyo Kiumwa amewaomba Madiwani kuendelea kusimamia miradi iliyop kwanye kata zao ili iweze kukamilika kwa wakati kwani amesema serikali inaendelea kushusha fedha kwa lengo ya kuwahudumia watanzania katika kuwaboreshea miundombinu ya afya,elimu na maji
sauti ya ally kiumwa 2
Aidha naye mwenyekiti wa halmashauri ya Busokelo Anyosisye Njobelo ameishukuru serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Mh,Samia Suluhu Hassani kwakuendelea kuipatia fedha halmashari ya Busokelo kwani amesema kwa robo ya kwanza ya mwaka kiasi cha shilingi Bilini 1na milioni mianane kwajili ya miradi mbalimbali
sauti ya Njobelo
Naye Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Rungwe ndg,Meckson Mwakipunga amesema chama cha mapinduzi kina imani na wataamu wanao simamia ilani ya chama hicho na kumtaka mkurugezi wa halmasharuri ya Busokelo kulipa madeni yanayodaiwa na wazabuni ili kuweka taarifa za fedha kama zinavyo takiwa kitaalam
sauti ya mwekiti wa ccm
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashari ya Busokelo Bi, Loema Peter amekiri kuwepo kwa changamoto iyp ya wazabuni kudai fedha amesema serikali imetoa fedha hivyo kufikia mwishoni mwa mwaka huu halmashari itakuwa imekamilisha kuwalipa fedha wazabuni hao
sauti ya mkurugenzi mtendaji