Chai FM

Mdau achangia zaidi ya shilingi milioni 38 maendeleo Rungwe

27 October 2024, 11:08 am

Viongozi wa dini wameombwa kuwa mstari wa mbele kukemea mmomonyoko wa maadili kwenye jamii

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Zaidi ya shilingi milioni 38 zimepatikana kwenye harambee ya kuchangia ununuzi wa gari aina ya coaster kwaji ya kwanya ya Watakatifu Petro na Paulo mitume ya kanisa la Roman catholic tukuyu mjini.

Awali kwanya hiyo ikisoma  risala yake mbele ya mgeni rasmi imetaja mafanikio iliyo yapata tangu kuazishwa kwake kuwa kwaya hiyo imekuwa ikiimarika siku hadi siku kiroho na kimwili pia kwaya imefanikiwa kuwa na maono ya kimaendeleo kwani imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni kumi na tano kwa dhumuni la ununuzi wa gari

Dr Mwafwenga[ kulia] alipokuwa akiwasili ukumbi wa kaninisa la Roma tukuyu aliwa ,geni rasmi kwenye harambee ya ununuzi wa basi

sauti ya risala 1

Mmoja wa wana kwaya akisoma risala mbele ya mgeni rasmi

 Hata hivyo kwanya imezitaja changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na wanakwanya kutokuwa na usafiri wa kusafiria,ukusanyaji ndogo wa michango kulinganga na kipato kidogo cha wanakwaya hiyo

sauti ya risala

Kwa upande wake mgeni rasmi Dr Samwel Mwafwenga ambaye ni mdau wa maendeleo wilani Rungwe amechangia kiasi cha shilingi Milioni kumi na Tano na   ameishukuru kwaya ya watakatifu Petro na Paulo Mitume  kwakuwa  na wazo ununuzi wa busi kwani pindi litakapo nunuliwa wataenda kupeleka injili sehemu mbalimbali na neon la Mungu litawafikia watu wote

sauti ya Dr mwafwenga 1

Dr,Mwafwenga amesema kutokana na maadili yalivyo poloka kwenye jamii ameiomba kwaya hiyo pindi watakapo kuwa wanahubiri injili wawakumbushe vijana kuwa na ofu ya mungu pamoja na kuliombea Taifa kwenye kipindi hiki cha uchaguzi

sauti ya Dr mwafwenga 2

Sambamba na hilo naye mwenyekiti wa kwaya amemshukuru mdau huyo wa maendeleo kwa kuwaunga mkono kwenye ununuzi wa basi kwani amesema linakwenda kupunguza baadhi ya changamoto

sauti ya mwnyekiti wa kwaya