Chai FM

Wananchi wameridhishwa na zoezi la uandikishaji Rungwe

11 October 2024, 4:18 pm

zoezi la uandikishaji kwenye daftari la mkazi kimeanza mapema hii leo octoba 11 hivyo kila wananchi unatakiwa kushiriki kikamilifu

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Wananchi wilayani Rungwe, mkoani Mbeya wametakiwa kijitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la mkazi ili waweze kuchagua viongozi watakao watumikia kwenye maeneo yao.

Wito huo umetolewa na katibu tawala wa wilaya rungwe Ally kiumwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati alipofika kwenye kituo alicho jiandikisha mapema hii leo kilichopo   chuo cha ualimu Tukuyu,

chifu Joel Mwakatumbula akishiriki zoezi la uandikishaji

sauti ya katibu tawala 1

Kiumwa amesema kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kushiriki zoezi la kujiandikisha katika daftari la mkazi kwani ndilo litakalompa nafasi ya kuchagua kiongozi anayemtaka.

Pia ameongeza kuwa ni haki ya msingi na ya kikatiba ya kila raia kushiriki zoezi la uchaguzi kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla.

sauti ya katibu tawala 2

kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Castory Makeula amesema zoezi la uwandikishaji linaendelea vizuri kwani wananchi wameitika kwa wingi kutokana na kila raia kujua umuhimu wa kupiga kura

sauti ya kaimu mkurugenzi

Naye chifu wa Mwakatumbula akiwa katika kituo kimoja wapo cha kujiandikisha amewaomba kwazi wa kijiji cha mbaka na wanarungwe kwa ujumla waende kwenye vituo vilivyopo kwenye maeneo yao ili waweze kujiandikisha kwenye daftari la mkazi

sauti ya mwakatumbula

Hata hivyo baadhi ya wananchi wamesema waliomefika kwenye vituo vya kujiandikishia wamesema wamefika hapo kwani ni haki yao kikatiba na kuwaomba wananchi wajiandikishe ili wweze kupiga kura ifikapo novemba 27

sauti za wananchi

Zoezi la uandikishaji limeanza rasmi mapema leo hii octoba 11,2024 na linatarajiwa kukamilika ifikapo octoba 20,2024 ,  ambapo halmashauri ya wilaya ya rungwe ina vituo vipatavyo miatano(500).