Chai FM

Zao la chai lapatiwa ufumbuzi Rungwe

10 October 2024, 5:46 pm

Ili kukboresha kipato cha mkulima mmojammoja wkulima wametakiwa kutolima kilimo cha mazoea waendane mabadiliko ya tabianchi

Na Bahati obeid

Afisa kilimo wilayani  Rungwe mkoani Mbeya Steven Mbiza amewataka wakulima  waliopata mafunzo ya shamba darasa kwenda kuwa mabalozi kwa wakulima wengine kwa mafunzo waliyo yapata ili kuongeza tija ya uzalishaji wa zao la chai

Ametoa wito huo wakati akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Rungwe kwenye mahafari ya wakulima hao ambao wamemaliza mafunzo yaliyofanyika katika amcos ya Rungwe ambapo amewataka wakulima pia kwnda kupanda miti 5 ya matunda ili kuepukana na udumavu 

sauti ya afisa kilimo

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wadogo wa chai mwenyekiti wa RBTC Issa Mwanyumba amewashukuru idh na washirika wengine kwa kuwezesha mafunzo hayo na misaada iliyotolewa kwenye ofisi za amcos huku akiwataka wakulima kuzingatia yale waliyojifunza.

sauti ya mwenyekiti wa RBTC

Naye Meneja IDH Tanzania Elikunda Tenga amesema kuwa wameweza kutengeneza madarasa 7143 kwa awam ya kwanza huku awam ya pili ikiwa na madarasa 13271 ambapo jumla ya wakulima 10266 ambao watahitimu kuanzia leo hadi tarehe 19 wiki ijayo

Afisa klimo wa wilaya akizungumza na wakulima

Sauti ya Meneja wa IDH