Chai FM

Viongozi wa vyama vya ushirika wamejengewa uwezo Rungwe

4 October 2024, 6:29 pm

vyama vya ushika vimetakiwa kuwa mstari wa mbele kusimamia maslai ya wakulima

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Ili kuhakikisha wakulima wanalima kilimo chenye tija wakulima wanao zalisha  mazao ya kahawa  na  kakao wilayani Rungwe wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa namna ya uzalishaji na usimamizi wa vya vyama vya msingi vilivyopo vyenye maeneo yao

Kauli hiyo imetolewa na afisa ushirika wilaya ndugu Tadei Mwambeso alipo kuwa akiwasilisha mada mbalimbali kwenye semina ya viongozi wa vyama vya ushirika semina iliyofanyka kwenye ukumbi wa Rungwe cooperative Union[RUCU] ulipo Tukuyu mjini

Mwambeso amebainisha lengo la semina hiyo kuwa ni kuwajengea uwezo  viongozi wapya waliochaguliwa wa vyama vya ushirika ambao ni mwenyeviti,makatibu pamoja na wajumbe wawe na uwezo wa kuwa tumikia wakulima

viongozi wa vyama vya ushirika wakisikilza mafunzo

sauti ya afisa ushirika

Kwa upande wao viongozi wa vyama hivo vya ushirika wameelezea faida walizo zipata kwe semina hiyo kwani wamesema wamefundishwa namna ya uwendeshaji wa ushirika uwapo kiongozi pamoja nakuwa mwazi katika mapato ya wanachama.

sauti za viongozi wa ushirika 1

Sambamba na hilo wamesema wamejifunza kuwa wadilifu kwa mali wanazo zisimamia pia wakulima wasilime kilimo cha mazoea wawe na utaratibu wa kupima udogo ili waweze kupata mazao mengi waweze kuimalika kiuchumi

sauti za .viongozi wa vyama vya ushirika 2