Barabara ya Lwangwa gesi kuinua uchumi wa wananchi Busokelo
3 October 2024, 6:08 pm
Ili kuinua uchumi wa wananchi serikali imejenga barabara ya kiwango cha lami kwa lengo la mkulima kuweza kusafirisha mazao yake kwa urahisi.
Na Lennox Mwamakula
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba John Kabudi ametembelea na kukagua mradi wa barabara ya Lwangwa-Kyejo inayojengwa kwa kiwango cha lami, iliyogharimu shilingi billion 6.1.
Waziri wa katba na sheria pro, Palamagamba kabudi akizungumza na wananchi wa Lwangwa[picha na Lennox Mwamakula]
Akizungumza na wananchi wa halmashauri ya wilaya ya busokelo katika eneo la soko la Ntangasale Lwangwa Mjini, Por Kabudi amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutarahisisha huduma ya usafirishaji kwa wananchi kutoka mazao yao kupeleka sokoni sambamba na kusambaza bidhaa na malighafi mbalimbali.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Busokelo akizungumza mbele ya waziri wa katiba na deria [picha na Lennox Mwamakula]
sauti ya waziri 1
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Busokelo Bi,Loema Peter amesema baada ya Barabara hiyo kukamilika itainua uchumi wa mtu mmoja mmoja na ukusasanji wa mapato utaongezeka kwani kwa kipindi kirefu wanachi walishindwa kupeleka mazao yao sokoni kutona na ubovu wa barabara hiyo kutoka mashambani
Mbunge wa jimbo la Busokelo Mh, Atupele Mwakibete akiongea kwa niaba ya wananchi ya jimbo lake [picha na Lennox Mwamakula]
sauti ya mkurugezi wa halmashauri
Aidha naye mbunge wa jimbo la Busokelo Mh,Atupele fredy Mwakibete ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha nyingi kwaajili ya miradi mbalimbali ikiwa ya Elimu,afya na maji kwani wananchi wanaedelea kupata matunda ya serikali yao
Hata hivyo Mwakibete amemuomba waziri kujenga soko kubwa katika eneo la Ntangasale kwani wajasiriamali hasa wakina mama wanashindwa kufanya biashara zao kwa uhuru kutokana na miundumbinu ya soko kuo kuwa rafiki
sauti ya mbunge wa jimbo la busokelo
Aidha waziri Kabudi amesema suala la ujenzi wa soko litafanyiwa kazi kwani mweshimiwa Rais samia suluju hasani ni kuwawekea mazingira rafiki wananchi ya kufanyia shughuli zao
sauti ya waziri 2
Nao wananchi ambao ni watumiaji wa barabara hiyo wamezunguuumzia adha waliokuwa wakikumbana nazo apo awali na wanaishukuru serikal kwa kuwajengea Barabara hiyo
sauti za wananchi