Baraza la wazee walia na pensheni Rungwe
2 October 2024, 8:13 pm
Katika kuadhimisha Siku ya Wazee Duniani wazee wameiomba serikali kuweka utaratibu wa kuyatambua mabaraza ya wazee nchini
NA Lennox Mwamakula
Baraza la Ushauri la Wazee wilaya ya Rungwe limeiomba serikali kuanzisha utaratibu maalum wa kuyatambua mabaraza ya wazee kuanzia ngazi ya vijiji, kata mkoa hadi ngazi ya kitaifa.
Wametoa kauli hiyo kwenye maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani ambayo kwa halmashauri ya wilaya ya Rungwe yamefanyika kwenye ukumbi wa halmashauri wa John Mwankenja zilipo ofisi za wilaya.
Kwa mujibu wa risala ya wazee, wamebainisha mafanikio pamoja na matarajio yaliyofanyika na baraza hilo kuwa ni pamoja na kuunda mabaraza kwenye kata ishirini na tano kati ya kata thelathini na tisa na wanatarajia kuzifikia kata zote ndani ya halmashauri ya wilaya ya Rungwe.
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Jaffar Hanniu akizungumza na wazee kwenye maadhimisho ya siku ya wazee duniani
Kuhusu mafanikio ya wazee
Hata hivyo wazee wamesema kwenye mafanikio hapakosi changamoto miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo ni kutokujua bajeti ya maadhimisho, kutokuwa na pensheni na kutokuwa na mfuko wa kuendeshea shughuli za baraza.
Kuhusu changamoto
Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku hiyo ya Wazee Duniani Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Jaffar Hanniu amewashauri wazee kuanzisha michango kutoka kwa wanachama pamoja na kutafuta wadau mbalimbali ili kuimarisha umoja huo ili uweze kujiendesha wakati serikali inaendelea kulifanyia kazi
Sauti ya Mkuu wa Wilaya
Sambamba na hilo mkuu huyo wa wilaya ya Rungwe ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wazee kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa serkali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu 2024
Sauti ya Mkuu wa Wilaya 2