Chai FM

Mwenge wa uhuru wakagua miradi ya bil.15 Rungwe

27 August 2024, 4:13 pm

Jamii imeshauriwa kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti rafiki ili kukabiliana ma mabadiliko ya tabianchi.

RUNGWE-MBEYA

Na Sabina Martin

Wananchi wilayani Rungwe mkoani Mbeya wametakiwa kujitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi wenye weledi na sifa siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwezi 11,mwaka huu 2024

Rai hiyo imetolewa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu ndg,Godfrey Mzava alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata ya Isongole kijiji cha Igweli wakati wa makabidhiano ya mwenge wa uhuru kwa halmshauri ya wilaya ya Rungwe ukitokea wilaya ya Mbarali.

Mwenge wa uhuru ulipo wasili kata ya isongole kijiji cha idweli halmashauri ya wilaya ya Rungwe ukitokea mbarali na kuukabidhi kwa mkuu wa wilaya ndg, Jaffar Hanniu

Aidha Mzava ametoa rai kwa wananchi na serikalikutunza mazingira kwa kupanda miti rafiki na kuondoa taka katika maeneoyasiyo rasmi huku akisisitiza ufugajiwenye tija kwa wananchi

Awali akitoa taarifa mkuu wa wilaya ya Rungwe Jaffar Hanniu amesema mwenge wa uhuru kwa halmashauri ya Rungwe utakimbizwa umbali wa kilometa 80.6 na kukagua miradi na kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwa miradi tisa yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 15.

Kauli mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka huu ni ’Tunza mazingira na shiriki ushaguzi wa serikali za mitaa kwa ujenzi wa taifa endelevu’